Social Icons

Tuesday, 21 November 2017

MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akizungumza Machache wakati wa Mahafali  ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy .Ambapo amewataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Urembo kwa kuwa ukuaji wake kwa sasa ni kubwa na inakabiliwa na Upungufu wa Wataalamu hivyo akiwashauri wanawake wengi Kujiunga na Kuiga Mambo Mazuri Yanayofanywa na Chuo cha Manjano Beauty Academy.Akieleza zaidi Alisema Sekta ya Urembo ina Fursa kubwa kwa Ajira kwa sasa,Katika Mahafali hayo  Wahitimu 120 Wametunukiwa vyeti katika  katika nyanja ya urembo.
Mwanzilishi wa Chuo cha  Manjano Beauty Academy Mama Shekha Nasser Akitoa Hotuba yake wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.Mama Shekha Nasser Amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwapeleka Watoto wao kwenye chuo hicho kwa LengoKupata Ujuzi wa Maswala ya Urembo,Aidha Ametaja Changamoto kubwa Alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho Ikiwemo ukosefu wa Wataalamu wazawa wa Maswala ya Urembo.
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akiwa na Wageni Waalikwa wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy 
 Baadhi ya  Wahitimu waliotunukiwa kwenye Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam

 Mshauri wa Maswala ya Kisaikolojia Anti Sadaka Akitoa Neno la Shukrani kwenye Mahafali hayo
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema  Akitoa Cheti kwa Mmoja wa Wahitimu Kwenye  Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy..
 Mgeni Rasmi,Uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy ,Wageni waalikwa na Wahitimu Wakiwa katika Picha ya Pamoja 

Chuo cha Manjano Beauty Academy  kimetunuku Astashahada (Certificates) na Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.Urembo na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi.
Wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha.


Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya  Manjano Beauty Academy iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha Manjano Beauty Academy.Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania.
“Tunashauri, tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,” alisema Shekha.Kwa mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi bora wanaopatikana katika sekta ya urembo  ambayo yatawatasaidia wao kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi.
 “Naamini kuwa wahitimu hawa watabadilisha sekta ya urembo hapa nchini, kama Korea na Filipino wanavyotambulika ulimwenguni kwa kuwa na bidhaa bora za ngozi na wataalam wa matibabu wenye weledi, huko mbeleni Tanzania itajulikana ni nchi inayotoa bidhaa bora za urembo kwa ngozi za Kiafrika, kuanzia bidhaa za urembo wa uso zinazozalishwa kutokana na Mwani wa baharini toka Zanzibar mpaka bidhaa za poda ambazo zina virutubisho vya Manjano ya asili na vyakutosha,” alisema Shekha ambaye pia ni mwanzilishi wa Shear Illusions.
Mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano, Shekha alizindua kampeni inayoitwa Manjano Dream Makers iliyokuwa na lengo la kuwawezesha wasichana wenye mafunzo ya kijasiriamali kujikwamua kiuchumi ili kutimiza ndoto zao.
“Katika miaka miwili tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Manjano, mtandao wa wanawake wa Manjano Dream-Makers umeweza kuenea katika majiji na miji Saba nchini na kuwasaidia kutengeneza ajira na kutengeneza kipato kwa kuuza bidhaa zao kupitia mfumo wa nyumba kwa nyumba kwa wanawake wasio na ajira,” alisema Shekha. 

Aliongeza kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 katika mtandao wa ‘Manjano Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.

Saturday, 18 November 2017

MWIGULU NCHEMBA AHITIMU SHAHADA YA UZAMIVU (PHD) UDSM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.  

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akiwa amepozi baada ya kumaliza hafla ya utoaji shahada hiyo.

Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na mtoto.
Waziri Nchemba akiteta jambo na wahitimu wenzake.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba leo amehitimu Shahada ya Uzamivu (PHD) ya Uchumi kwenye Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo mahafali hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar. Mahafali hayo yalihudhuriwa na mkuu wa chuo hicho ambaye ni rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAHAFALI YA 10 YA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU (DUCE) CHA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, (pichani juu), ameongoza mahafali ya kumi (10), ya  Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo kikuu Dar es salaam kwenye viwanja vya chuo hicho, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2017.
Katika mahafali hayo zaidi ya wanachuo 1,443 waliochukua mafunzo ya Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED), Shahada ya Elimu ya Sayansi na Elimu, (Bsc) na Shahada ya Elimu (BED), pamoja na wahitimu waliojiendeleza (Post graduate), 
walitunukiwa shahada ya kwanza, ambapo mwanachuo Dadi Omary Safari, alipewa tuzo ya kuwa mwanachuo bora zaidi kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED) Amisa Hassan.
Baadhi ya wahitimu katika mahafali ya 10 ya ya  Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo kikuu Dar es salaamwakiwa kwenye mahafali hayo
Furahaya kuhitimu na kutunukiwa shahada.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, akisoma hotuba yake.
Dkt. Kikwete, akipitia ratiba ya mahafali hayo.
Dkt. Kikwete akitangaza kuwatunuku shahada baadhi ya wanachuo hao.
Baadhi ya wanachuo wakisubiri kutunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Dkt. Kikwete, akiteta jambo na Profesa Mukandala.
Dkt. Kikwete, akiipitia tuzo ya mwanachuo bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari kabla ya kumkabidhi.
Mwanachho bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari akiwa na tuzo yake.
 
Dkt. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wahitimu, Amisa Hassan, na baba mdogo wa muhitiumu huyo, Khalfan Said.

Thursday, 16 November 2017

MAHAFALI DUCE YAFANA, PROF MUKANDALA AWAAGA RASMI WANA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
 
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewatunukia wahitimu 1443 wa ngazi mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es salaam (DUCE) kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Katika mahafali hayo Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete aliwatunukia wahitimu hao sambamba na kutoa zawadi kwa wanafunzi nane waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.

Rais wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam, Prof William Anangiyse amesema kuwa jumla ya wahitimu 1371 wametunukiwa digrii za awali katika fani mbalimbali na Wahitimu 72 ni wa ngazi ya stashahada ya uzamili katika elimu  (PGDE) na kutimiza idadi ya 1443.

Prof Anangisye amesema kuwa jumla ya 928 ni wanaume na 515 ni wanawake huku wahitimu 1015 wakitunukiwa digrii ya elimu ya jamii na ualimu (B.A.Ed), , 233 ni wahitimu wa Sayansi na Ualimu ( B.Sc.Ed), wahitimu 72 ni Elimu katika sayansi (B.Ed.Science) na Elimu katika elimu ya Jamii ( B.Ed.Arts) ni wahitimu 51.
Mbali na hilo, Mwenyekiti wa bodi ya Usimamizi ya Chuo Kikuu Kishirikishi  Cha Elimu Dar es Saalam, Prof. Rwekaza Mukandala kwenye mahafali ya 10 ya chuo hicho amewaaga rasmi wanajumuiya wa Chuo Kikuu Kishirikishi  baada ya kumaliza muda wake wa mwaka mmoja alioongezewa na Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwenhe mahafali ya mwaka jana.

Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete aliweza kutoa zawadi kwa wahitimu nane waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho pamoja na Emanuel Safari Dadi aliyefanya vizuri kwa ujumla na kumpongeza kwa juhudi kubwa alizozifanya katika kipindi chake cha masomo.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepiga picha na mhitimu Emanuel Safari Dadi aliyefanya vizuri katika mitihani yake yote na kupata GPA 5.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu  Dar es Salaam Peter Ngumbulu (Kulia), Rais wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam Prof William Anangyse, Mlau wa Chuo Kikuu Kishirikishi Cha Elimu Dar es Salaam Prof. Martha Qorro na wajumbe wengine katika mahafali ya 10 yaliyofanyika jana Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa zawadi kwa wahitimu nane waliofanya vizuri kwenye mitihani yao. Chini akiwa amepiga nao picha ya pamoja.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunukia wahitimu wa ngazi mbalimbali katika mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika jana Jijinj Dar es Salaam.

Wednesday, 15 November 2017

VIONGOZI TAASISI FEKI MIKOPO ELIMU YA JUU MBARONI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

Imeandikwa na Magnus Mahenge, 
Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Tanzania Social Support Foundation (TSSF) Donati Salla (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kutiwa mbaroni jana
SERIKALI imeviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kulichunguza Shirika la Tanzania Social Support Foundation (TSSF) kutokana na kudaiwa kuwahadaa Watanzania linatoa mikopo na wanafunzi 198 wakarubuniwa kwamba watapewa mikopo ya zaidi ya Sh milioni 533.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, William Ole Nasha pia amepiga marufuku shirika hilo kujihusisha na utoaji mikopo na amezifunga akaunti zake zote baada ya kujiridhisha hakuna hata chembe ya shirika hilo kuwa na uwezo wa kutoa mikopo.
“Naviagiza vyombo vya usalama kuwakamata na kuwahoji viongozi wa shirika hili, kuwauliza ukweli kuhusu huduma za utoaji mikopo na kujiridhisha kuhusu mkakati wa kuwaibia na sheria ichukue mkondo wake,” alisema Waziri.
Alisema shirika hilo ni la kitapeli kutokana na kuwatoza wanafunzi Sh 30,000 kila mmoja za kujisajili wakati haina fedha kwenye akaunti. Alisema viongozi wa shirika hilo wamesema walitegemea kupata fedha kutoka Kampuni ya Cagney la Marekani ambapo kwanza walitakiwa kutoa dola 50,000 ili wawape ufadhili huo.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Donati Salla alikiri kuwatoza wanafunzi Sh 30,000 na akaahidi kuzirudisha mapema Serikali itakavyoagiza na wapo tayari kuendelea kutoa usajili bure kwa wanafunzi kwa lengo la kuwasaidia Watanzania.
Ofisa Utawala, Marwa Charles alisema shirika lao si la kiserikali, hivyo si lazima liwe na fedha linapotoa huduma na si lazima lioneshe kiwango cha fedha kilicho benki bali linatoa huduma tu.
Charles alisema kulikuwa na matatizo katika shirika hivyo wakachelewa kutuma dola 50,000 za Marekani sawa na Sh milioni 112 Novemba 12, mwaka huu nchini Marekani ili wapate fedha za kukopesha wanafunzi 50,000.
Waziri Ole Nasha alisema shirika hilo ni la kitapeli kwa sababu limetumia fursa ya uhitaji wa mikopo kwa wanafunzi kudanganya ambapo wanafunzi 600 waliomba mikopo wakati likijua halina fedha zaidi ya Sh milioni 60 au 70 tu.
“Shirika hilo ni la kitapeli”, Ole Nasha alisema na kuongeza katika mkataba na Kampuni ya The Cagney ya Marekani, hakuna mahali popote palipoonesha itatoa fedha kuwafadhili wanafunzi, badala yake viongozi walikuwa wakiulizia uwezekano wa kufanya harambee.
Waziri ole Nasha alisema katika mkutano na viongozi wa taasisi hiyo, alisema wamebaini TSSF haina uwezo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi 50,000, bali ulikuwa utapeli wa kupata Sh 30,000 za ada za kujiandikisha.
Alisema hakuna sehemu ya kupata fedha na serikali inatoa taarifa kwa umma ufahamu shirika hilo halina uwezo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi waliokwishaanza masomo vyuoni wakitegemea kupata mikopo Desemba 20, 2017.
Japo taasisi hiyo ilisajiliwa kihalali nchini, serikali imebaini kwamba bajeti yake kwa mwaka ni Sh milioni 2.5, hivyo kusingekuwa na miujiza kuwa na uwezo wa kuwa na fedha za kutosha kufadhili wanafunzi 50,000 kwani historia haioneshi uwezo huo wa kifedha.
Alisema shirika hilo lilikuwa na nia mbaya ya kuwahadaa wanafunzi na lilidai wangekosa fedha Marekani, wangepata China ambako pia hakuna mkataba wa makubaliano ya fedha.
Wanafunzi 198 walioahidiwa mikopo na shirika hilo walikuwa wameomba kusoma vyuo vikuu vya Dar es Salaam (UDSM), Nyegezi (SAUT), Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (MUHAS), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro na vingine walitozwa Sh 30,000 za kusajiliwa jumla yake ikiwa Sh milioni 5.94.
Kutokana na uhaba wa mikopo ya wanafunzi katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), zaidi ya wanafunzi 600 walikuwa wameahidiwa watapewa mikopo na shirika hilo na kurudisha fedha kwa riba ya asilimia sita.
Naibu Waziri ole Nasha alisema, serikali itaangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi hao waliotapeliwa na shirika hilo kwani wanaweza kushindwa kuendelea na masomo yao kwa sasa.
Mkutano na waandishi wa habari ulipomalizika, viongozi wa shirika hilo, Salla na Charles walikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi kwenda kutoa maelezo kuhusu nia hiyo ya kutapeli wanafunzi wenye shida ya mikopo.
CHANZO HABARI LEO

Monday, 13 November 2017

WALIOKOPESHA WANAFUNZI VYUO VIKUU WAJITETEA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

 Imeandikwa na Isdory Kitunda
SHIRIKA la Maendeleo ya Kijamii nchini (TSSF) limesema kuwa linafanya kazi zake kihalali na kuwa kesho asubuhi litawasilisha nakala za uhalali wake huo kwenye Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mwishoni mwa wiki, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako katika Mkutano wa Bunge unaoendelea Dodoma, akimjibu Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi aliyeomba mwongozo kuhusu uhakika wa TSSF katika kutoa mikopo nafuu kwa wanafunzi wa elimu ya juu, alikana kulifahamu na kutaka watu kulipuuza.
Kutokana na kauli hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TSSF, Donati Salla, jana alitoa taarifa akisema kesho ataenda wizarani kujielezea kuhusu uendeshwaji wa shughuli zake hizo akiwa na nakala muhimu za shirika hilo.
Salla alisema hadi jana hakuwa amepewa barua rasmi ya kumtaka kuripoti, lakini hata hivyo alisema kwa sasa shirika lake halina mrejesho wa kusema dhidi ya tamko la Waziri Ndalichako kuhusu yeye na wizara yake kutoitambua TSSF licha ya shirika hilo kufanya jitihada mbalimbali za kujitambulisha kwa wizara.
CHANZO HABARI LEO

BODI YATAJA 1,775 ZAIDI MIKOPO VYUO VIKUU

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

 Imeandikwa na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdul-razaq Badru
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetangaza orodha nyingine ya wanafunzi 1,775 wa mwaka wa kwanza huku ikifungua dirisha la rufaa hadi Novemba 19, mwaka huu.
Kutolewa kwa orodha ya wanafunzi 1,775 waliopata mikopo, kunafanya jumla ya wanafunzi 31,353 waliopewa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza pekee. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitangaza majina ya wanafunzi 10,196, awamu ya pili wanafunzi 11,481 na awamu ya tatu wanufaika 7,901. Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdul-razaq Badru (pichani) katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Badru alisema orodha na majina iliyotolewa tayari imeshatumwa kwa vyuo husika ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo. “Tumekuwa tukifanyia kazi orodha za udahili ambazo tumekuwa tukipokea, na kila tunapokamilisha, tunatoa orodha za wanafunzi waliopangiwa mikopo ambao wana sifa, leo (jana) tumetoa majina ya wanafunzi 1,775,” alisema Badru.
Serikali imetenga Sh bilioni 427.54 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa Sh bilioni 147.06 kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu. Katika fedha hizo, Sh bilioni 427.54, ni kwa ajili ya wanafunzi 122,623 wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo.
Akizungumzia kufunguliwa kwa dirisha la rufaa, Badru alisema bodi imefungua dirisha la rufaa kuanzia leo hadi Novemba 19, mwaka huu ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili.
“Lengo la HESLB ni kuhakikisha wanatangaza orodha ya majina ya waombaji mikopo waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo au kabla ya Novemba 30, mwaka huu. “Tunatoa mwito kwa uongozi wa vyuo vyote kupokea maombi ya rufaa za wanafunzi na kuwasilisha kwa bodi ya mikopo kabla ya Novemba 22 mwaka huu ili kuiwezesha bodi kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo Novemba 30,” alieleza.
Hivi karibuni, HELSB ilisema wanafunzi ambao hawakupangiwa mkopo ni pamoja na waliokuwa na udahili chuo kikuu zaidi ya kimoja na waliothibitisha awali wakitaja chuo watakachokwenda lakini baadaye wakabadilisha.
Kundi lingine la waliokosa mikopo ni pamoja na waliowasilisha maombi yakiwa na dosari kadha wa kadhaa na wengine wakiwa na sifa pungufu za uhitaji wa mkopo. Kutokana na malalamiko ya wanafunzi waliokosa mikopo, bodi iliahidi kufungua dirisha la rufaa ya kupata mikopo ili kuwapa fursa wanafunzi ambao hawajaridhika kuwasilisha rufaa zao kupitia vyuo walivyopata udahili na majina ya watakaofanikiwa kupata mikopo yatatolewa.
CHANZO HABARI LEO 

Friday, 10 November 2017

VYUO VISUMBUFU MIKOPO YA WANAFUNZI KUFUNGIWA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
 Imeandikwa na Maulid Ahmed, Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo wa Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
SERIKALI imeviagiza vyuo vyote vya elimu ya juu kusajili wanafunzi, kuwapatia fedha zao za mikopo na watakaowasumbua watafungiwa.
Aidha imesema mpaka sasa wanafunzi 29,578 wa mwaka wa kwanza wameshapelekewa fedha zao za mikopo walikodahiliwa. Hayo yalibainishwa jana bungeni na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu udahili na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2017/2018.
Kauli hiyo ilitokana na Bunge kuiagiza serikali kutoa kauli kuhusu udahili na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi hao kutokana na mwongozo wa Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata (CCM).
“Serikali haitasita kuchukua hatua kali ikiwemo kuvifungia vyuo vitakavyoleta usumbufu usio wa lazima kwa wanafunzi na kuwafanya wapoteze muda ambao wanapaswa wautumie kwa masomo, UDOM (Chuo Kikuu cha Dodoma) na Chuo cha Mwalimu Nyerere wana urasimu kupokea wanafunzi, Chuo Kikuu Mwenge nimeona kinawalazimisha wanafunzi kubadilisha kozi na wanawaambia kozi zimejaa wakati waliomba na wakapata...tutavifungia vyuo vyote vinavyosumbua wanafunzi na kuwafanya wawe wazururaji mitaani,” alisema.
Profesa Ndalichako ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Kurugenzi ya Elimu ya Juu ya Wizara ya Elimu kufuatilia kwa karibu mambo yanayoendelea vyuoni wakati wanafunzi wanaripoti na kuwabainisha wote wanaokiuka taratibu na kuwanyima wanafunzi haki yao ya kusoma programu wanazotaka.
Alisema kwa wanafunzi walioripoti vyuo tofauti na mikopo yao iliyopelekwa vyuo vingine, mikopo yao itahamishiwa kwenye vyuo walivyodahiliwa baada ya kupokea uthibitisho kutoka katika vyuo vilivyowapokea.
Alisema hadi Novemba 07 wanafunzi 29,578 wa mwaka kwanza walikuwa wamepangiwa mikopo kati ya wanafunzi 30,000 wanaostahili. Alisema serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Ellimu ya Juu imepanga kutumia Sh bilioni 427.54 kugharamia mikopo kwa wanafunzi 122,623 ambapo 30,000 ni wa mwaka wa kwanza na 92,623 ni wanaoendelea na masomo.
Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, Wizara ya Elimu imepokea Sh bilioni 147.06 kwa ajili ya ada za wanafunzi hao kugharamia chakula, malazi, vitabu, viandikia na mahitaji ya masomo.
CHANZO HABARI LEO

Thursday, 9 November 2017

“TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
JUMUIYA wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) wameiangukia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB) kuharakisha fedha za wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo kwa kupata alama D waliopo vyuoni(supplementary).

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Stanslaus Kadugalize wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema idadi ya wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo vyuoni ni kubwa na mpaka sasa hawajapata fedha za kujikimu .

Alisema fedha hizo ni kama kauli ya Naibu Waziri wa Elimu alivyosema kuwa ifikapo ijumaa wiki iliyopitia fedha ziwe zimefika vyuoni lakini mpaka sasa fedha hizo hazijafika jambo ambalo linawapa wakati mgumu wanafunzi hao.

Mwenyekiti huyo alivitaka vyuo visiweke sababu zisizo za msingi juu ya kuwapa wanafunzi fedha zao za kujikimu kwa wale ambao tayari fedha zimekwisha fikishwa vyuoni kwa kigezo cha kujisajili.

“Tunatambua umuhimu wa kujisajili ila vyuo vitambue pia kwamba wapo wanafunzi wengi wanategemea fedha hizo hizo za bodi ya mikopo (HESLB) ili kulipia gharama za kujisajili kuweza kukamilisha zoezi la kujisajili hivyo vyuo viache kuweka sababu zinazopelekea usumbufu kwa wanafunzi “Alisema.

Kuhusu zoezi la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza alisema sasa bodi ya hiyo imekwisha kutoa kwa wanafunzi 29,000 kwa wale wote ambao wanasifa na hawajapata katika upangaji wa awali aliwashauri kutumia dirisha la rufani linalofunguliwa Novemba 13 mwaka huu ambapo rufaa hizo itakuwa ni bure.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo hakisita kuzungumzia kuhusu zoezi la udahili ambapo ambapo aliitaka TCU kuingilia kati kwani bado kuna usumbufu mkubwa wa wanafunzi wanaoupata na una hatarisha baadhi yao kukosa nafasi ya kusoma.

Alisema vipo vyuo vimefahili wanafunzi zaidi ya idadi wanayotakiwa mfano chuo cha Mwenge na vyenginevyo jambo la ajabu wanapokwenda kuripoti vyuoni wanaambiwa wamekwisha kamilisha idadi walizopangiwa.

“Sasa tunajiuliza kwanini walikubali idadi kubwa ya wanafunzi
wathibitishe kwenye vyuo vyao? kwanini wasiweke ukomo wa idadi kulingana na wanayotakiwa  lakini pia mpaka sasa wapo wanasumbuliwa vyuoni hawajapokelewa na wametoka makwao “Alisema.

“Mfano yupo mwanafunzi ametoka kwao Arusha amekwenda Mwanza kuripoti chuo kalipa na ada kabisa ya chuo sikitaji  na alithibitisha kusoma hapo ajabu amekwenda kuripoti wana mwambia wameshajaza idadi hivyo subiri maamuzi ya TCU kama wataruhusu kuwapokea “Alisema.

Aliongeza kuwa vyuo visipelekee vurugu zisizo na maana yoyote ile endapo wanafunzi hao watakosa nafasi za masomo kwa mwaka huu kwa uzembe wa vyuo kudahili zaidi ya idadi yao kwa hofu ya kukosa wanafunzi .

“Lakini niwaambie sisi kama Tahliso hatutasita kuvichukulia hatua vyuo hivyo kwa kuwalipa fidia ya usumbufu wanafunzi  ambao wamekumbana naowakati wa kufuatilia michakato hiyo “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha