Social Icons

Wednesday 1 October 2014

HATARI : PROFESA WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) AFARIKI KWA KUPIGWA NA RISASI



Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana.

Profesa Mukandala alisema Profesa Livigha alikutwa na masaibu hayo akiwa nyumbani kwake Bunju, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana na kwamba, mwili wake umechukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

“Ni kweli, na mimi hizo habari tumezipata na watu wote wamekwenda nyumbani kwake. Mwili umechukuliwa na polisi, tunasubiri taarifa kutoka polisi,” alisema Profesa Mukandala bila kufafanua zaidi.

Aliongeza: “Mimi nilikuwa mjini, wenzangu wamekwenda nyumbani kwake Bunju. Tumesikitishwa sana kwa kupotelewa na mwalimu wetu mwingine katika mazingira kama hayo.”

Profesa mwingine wa UDSM, Jwani Kwaikusa, aliuawa Julai, 2010 kwa kupigwa risasi na watu waliodaiwa kuwa ni majambazi.


Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: