Social Icons

Featured Posts

Tuesday, 21 November 2017

NGONGAMANO LA WASOMI WANATAALUMA KUFANYIKA JUMAMOSI HOTELI YA LANDMARK UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

 Mratibu wa Kongamamo la Wasomi Wanataaluma wa Kikristo liitwalo Tanzania for Jesus Prayer Movement ambalo mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus,  Ephrahim Mwambapa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Kanisa la Abundant Bressing Center (ABC), Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo litakalofanyika Hoteli ya Landmark siku ya Jumamosi. Kulia ni Mjumbe wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli.

Mratibu wa Kongamano hilo, Ephrahim Mwambapa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

Na Dotto Mwaibale

WANAFUNZI waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini Jumamosi ya Wiki hii wanatarajia kufanya kongamono kubwa la kihistoria kujadili namna watakavyoweza kutumia taaluma zao kusaidia jamii, kanisa na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mratibu wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.

Alisema licha ya muungano huo kuundwa na vijana wa kikristo lakini vijana wote wasomi kutoka katika vyuo na shule za sekondari na madhehebu mbalimbali wanaalikwa ili kuchangia mada zitakazo jadiliwa na mgeni rasmi atakuwa ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

Mwambapa alisema kuwa katika kongamano hilo kutakuwepo na mada mbalimbali na kuona ni jinsi gani kila mmoja na taaluma yake ataweza kusaidia jamii badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kuifanyia kazi.

"Tunapokuwa vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii na ndio maana tumeona ni vizurio kuazisha muungano huu lengo likiwa kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema Mwambapa.

Alisema wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano ya mkutano mkuu wa kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mwambapa alisema kongamano hilo litafanyika Hoteli ya Landmark Ubungo jijini Dar es Salaam na litahudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali,sekondari baadhi wa viongozi.

MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHAZILI TABORA AKUTWA AMEJINYONGA KWA KUTUMIA TAI.

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
21 November 2017.
MWANACHUO mmoja Chuo cha Utumishi wa Umma –Tawi la Tabora kinachojulikana kama Uhazili  Raphael Kadesha (22)  amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai ya kuvaa shingoni.
 
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Graifton Mushi tukio hilo limetokea leo saa 4 asubuhi ambapo marehemu alifunga tai juu ya kitanda chake.
 
Alisema kuwa marehemu alikuwa akisoma kozi cha Cheti cha Awali cha Utawala katika Chuo hicho.
 
Mushi aliongeza kuwa chanzo cha kifo hicho hakijulikani na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kujua nini kilimfanya mwanachuo huyo kuchukua maamuzi hayo yaliyoacha simanzi katika jamii yake na Chuo kwa ujumla.
 
Alitoa wito kwa wanachuoni kuomba ushauri kwa viongozi wao Chuo au wa kiroho pindi wanapokuwa na matatizo binafisi kwani kujiua sio suluhisho la matatizo bali ni kuwaongezea walezi wao shida na majonzi zaidi.
Mushi alisema kuwa mwili wa marehemu umehifahiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete.
Naye Mkurugenzi wa  Chuo hicho Dkt. Ramadhani Marijani alitoa wito kwa wanachuo kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa sababu zilizopelekea mwanachuo huyo kuchukua maamuzi yaliyoacha simamazi sio tu kwa familia yake bali hata kwa Jumuiya nzima ya Uhazili.
Alisema kuwa ni vema kama kuna mwanachuo yoyote anakuwa na tatizo au msongo wa mawazo kuwaeleza viongozi wake wawe wa Serikali ya Wanafunzi, Mama Mlenzi, Mshauri wa Wanachuo au Mkurugenzi mwenye ili waweze kusaidia katika ushauri utakaowapa ufumbuzi kuliko kuchukua maamuzi ya haraka.

CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI YAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Katibu Mkuu Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Florens Turuka akisalimia na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddy Kimanta
mara  baada ya kuwasili katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Mondoli(TMA) kwa ajili ya uzinduzi wa shahada ya kwanza ya mafunzo ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo leo(Picha na Pamela Mollel Arusha)

  Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania Jenerali Vanance Mabeyo  akisalimiana na Kaimu Mkuu wa  chuo cha uhasibu Arusha Dokt Faraji Kasidi, katikati ni Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao 

Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Florens Turuka akisalimia Generali Maj Othaman
mara  ya kuwasili katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Mondoli(TMA) kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo


Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka akisalimiana na Dr. Adolf B. Rutayuga ambaye ni kaimu mtendaji mkuu wa NACTE.

Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka akizungumza katika uzinduzi wa  uzinduzi wa shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo


Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akitoa hotuba fupi katika halfa ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo


 Meja jenerali Paul Peter Masao ambaye ni mkuu wa chuo cha mafunzo ya maafisa wanafunzi jeshi la ulinzi la Tanzania(TMA).

 Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha uhasibu Arusha Bi.Rukia Adam akisoma maelezo mafupi  juu ya uzinduzi wa wafunzo ya shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA). 


Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo  alisema mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia.
 

kushoto aliyevalia suti ni Profesa Johannes Monyoambaye aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha(IAA)
 Wanafunzi  wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo leo
Maafisa wa jeshi wakitumbuiza wata wa uzinduzi wa wafunzo ya sayansi ya kijeshi.
 Picha ya pamoja


Na Pamela Mollel,Monduli

Katibu Mkuu wa wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dokta Florens Turuka amesema kuwa jeshi hilo hivi sasa limejipanga katika kukabiliana na changamoto za ulinzi na usalama kwa kuwapatia askari wake mafunzo maalumu ya sayansi ya kijeshi. 

Aliyasema hayo Jana wakati akizungumza katika uzinduzi wa shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA). 

Alisema kuwa, kumekuwepo na matishio mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza Kwa namna tofauti ambapo hivi sasa matishio hayo yamegeuka na kuhamia kwenye mitandao, hivyo kama jeshi wana wajibu wa kujipanga zaidi kwa kuwaandaa maaskari ili waweze kukabiliana na hali hiyo mahali popote. 

Dokta Turuka alisema kuwa, wao Kama jeshi ni wajibu wao kujipanga mapema kwa kuangalia namna ya kuwajengea uwezo hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia ili kuboresha ulinzi na usalama hapa nchini. 

Kwa upande wa Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo alisema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo hayo kwa maaskari wake kulingana na mabadiliko ya kidunia hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia kwani ni eneo ambalo linahitaji elimu kubwa zaidi. 

Alisema kuwa, ni lazima wasonge mbele na kwenda na wakati kwani wasipofanya hivyo watabaki nyuma na kamwe hawataweza kukabiliana na vitisho vilivyopo  hivi sasa. 

Naye Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao alisema kuwa, wamekuwa wakitoa masomo ya kijeshi na kiraia ili kuwaandaa vijana katika hatua ya ngazi za  juu zaidi  kielimu  ambapo kwa kuanzia kozi hiyo watahiniwa  158  wataanza kozi hiyo mapema. 


Kwa upande wa Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi alisema kuwa, mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia ambayo yamekuwa yakileta manufaa makubwa Sana. 

Mwisho. MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akizungumza Machache wakati wa Mahafali  ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy .Ambapo amewataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Urembo kwa kuwa ukuaji wake kwa sasa ni kubwa na inakabiliwa na Upungufu wa Wataalamu hivyo akiwashauri wanawake wengi Kujiunga na Kuiga Mambo Mazuri Yanayofanywa na Chuo cha Manjano Beauty Academy.Akieleza zaidi Alisema Sekta ya Urembo ina Fursa kubwa kwa Ajira kwa sasa,Katika Mahafali hayo  Wahitimu 120 Wametunukiwa vyeti katika  katika nyanja ya urembo.
Mwanzilishi wa Chuo cha  Manjano Beauty Academy Mama Shekha Nasser Akitoa Hotuba yake wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.Mama Shekha Nasser Amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwapeleka Watoto wao kwenye chuo hicho kwa LengoKupata Ujuzi wa Maswala ya Urembo,Aidha Ametaja Changamoto kubwa Alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho Ikiwemo ukosefu wa Wataalamu wazawa wa Maswala ya Urembo.
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akiwa na Wageni Waalikwa wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy 
 Baadhi ya  Wahitimu waliotunukiwa kwenye Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam

 Mshauri wa Maswala ya Kisaikolojia Anti Sadaka Akitoa Neno la Shukrani kwenye Mahafali hayo
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema  Akitoa Cheti kwa Mmoja wa Wahitimu Kwenye  Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy..
 Mgeni Rasmi,Uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy ,Wageni waalikwa na Wahitimu Wakiwa katika Picha ya Pamoja 

Chuo cha Manjano Beauty Academy  kimetunuku Astashahada (Certificates) na Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.Urembo na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi.
Wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha.


Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya  Manjano Beauty Academy iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha Manjano Beauty Academy.Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania.
“Tunashauri, tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,” alisema Shekha.Kwa mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi bora wanaopatikana katika sekta ya urembo  ambayo yatawatasaidia wao kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi.
 “Naamini kuwa wahitimu hawa watabadilisha sekta ya urembo hapa nchini, kama Korea na Filipino wanavyotambulika ulimwenguni kwa kuwa na bidhaa bora za ngozi na wataalam wa matibabu wenye weledi, huko mbeleni Tanzania itajulikana ni nchi inayotoa bidhaa bora za urembo kwa ngozi za Kiafrika, kuanzia bidhaa za urembo wa uso zinazozalishwa kutokana na Mwani wa baharini toka Zanzibar mpaka bidhaa za poda ambazo zina virutubisho vya Manjano ya asili na vyakutosha,” alisema Shekha ambaye pia ni mwanzilishi wa Shear Illusions.
Mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano, Shekha alizindua kampeni inayoitwa Manjano Dream Makers iliyokuwa na lengo la kuwawezesha wasichana wenye mafunzo ya kijasiriamali kujikwamua kiuchumi ili kutimiza ndoto zao.
“Katika miaka miwili tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Manjano, mtandao wa wanawake wa Manjano Dream-Makers umeweza kuenea katika majiji na miji Saba nchini na kuwasaidia kutengeneza ajira na kutengeneza kipato kwa kuuza bidhaa zao kupitia mfumo wa nyumba kwa nyumba kwa wanawake wasio na ajira,” alisema Shekha. 

Aliongeza kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 katika mtandao wa ‘Manjano Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.

Saturday, 18 November 2017

MWIGULU NCHEMBA AHITIMU SHAHADA YA UZAMIVU (PHD) UDSM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.  

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akiwa amepozi baada ya kumaliza hafla ya utoaji shahada hiyo.

Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na mtoto.
Waziri Nchemba akiteta jambo na wahitimu wenzake.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba leo amehitimu Shahada ya Uzamivu (PHD) ya Uchumi kwenye Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo mahafali hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar. Mahafali hayo yalihudhuriwa na mkuu wa chuo hicho ambaye ni rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAHAFALI YA 10 YA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU (DUCE) CHA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, (pichani juu), ameongoza mahafali ya kumi (10), ya  Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo kikuu Dar es salaam kwenye viwanja vya chuo hicho, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2017.
Katika mahafali hayo zaidi ya wanachuo 1,443 waliochukua mafunzo ya Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED), Shahada ya Elimu ya Sayansi na Elimu, (Bsc) na Shahada ya Elimu (BED), pamoja na wahitimu waliojiendeleza (Post graduate), 
walitunukiwa shahada ya kwanza, ambapo mwanachuo Dadi Omary Safari, alipewa tuzo ya kuwa mwanachuo bora zaidi kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED) Amisa Hassan.
Baadhi ya wahitimu katika mahafali ya 10 ya ya  Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo kikuu Dar es salaamwakiwa kwenye mahafali hayo
Furahaya kuhitimu na kutunukiwa shahada.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, akisoma hotuba yake.
Dkt. Kikwete, akipitia ratiba ya mahafali hayo.
Dkt. Kikwete akitangaza kuwatunuku shahada baadhi ya wanachuo hao.
Baadhi ya wanachuo wakisubiri kutunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Dkt. Kikwete, akiteta jambo na Profesa Mukandala.
Dkt. Kikwete, akiipitia tuzo ya mwanachuo bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari kabla ya kumkabidhi.
Mwanachho bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari akiwa na tuzo yake.
 
Dkt. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wahitimu, Amisa Hassan, na baba mdogo wa muhitiumu huyo, Khalfan Said.

Thursday, 16 November 2017

MAHAFALI DUCE YAFANA, PROF MUKANDALA AWAAGA RASMI WANA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
 
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewatunukia wahitimu 1443 wa ngazi mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es salaam (DUCE) kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Katika mahafali hayo Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete aliwatunukia wahitimu hao sambamba na kutoa zawadi kwa wanafunzi nane waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.

Rais wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam, Prof William Anangiyse amesema kuwa jumla ya wahitimu 1371 wametunukiwa digrii za awali katika fani mbalimbali na Wahitimu 72 ni wa ngazi ya stashahada ya uzamili katika elimu  (PGDE) na kutimiza idadi ya 1443.

Prof Anangisye amesema kuwa jumla ya 928 ni wanaume na 515 ni wanawake huku wahitimu 1015 wakitunukiwa digrii ya elimu ya jamii na ualimu (B.A.Ed), , 233 ni wahitimu wa Sayansi na Ualimu ( B.Sc.Ed), wahitimu 72 ni Elimu katika sayansi (B.Ed.Science) na Elimu katika elimu ya Jamii ( B.Ed.Arts) ni wahitimu 51.
Mbali na hilo, Mwenyekiti wa bodi ya Usimamizi ya Chuo Kikuu Kishirikishi  Cha Elimu Dar es Saalam, Prof. Rwekaza Mukandala kwenye mahafali ya 10 ya chuo hicho amewaaga rasmi wanajumuiya wa Chuo Kikuu Kishirikishi  baada ya kumaliza muda wake wa mwaka mmoja alioongezewa na Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwenhe mahafali ya mwaka jana.

Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete aliweza kutoa zawadi kwa wahitimu nane waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho pamoja na Emanuel Safari Dadi aliyefanya vizuri kwa ujumla na kumpongeza kwa juhudi kubwa alizozifanya katika kipindi chake cha masomo.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepiga picha na mhitimu Emanuel Safari Dadi aliyefanya vizuri katika mitihani yake yote na kupata GPA 5.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu  Dar es Salaam Peter Ngumbulu (Kulia), Rais wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam Prof William Anangyse, Mlau wa Chuo Kikuu Kishirikishi Cha Elimu Dar es Salaam Prof. Martha Qorro na wajumbe wengine katika mahafali ya 10 yaliyofanyika jana Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa zawadi kwa wahitimu nane waliofanya vizuri kwenye mitihani yao. Chini akiwa amepiga nao picha ya pamoja.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunukia wahitimu wa ngazi mbalimbali katika mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika jana Jijinj Dar es Salaam.