Social Icons

Tuesday, 21 November 2017

CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI YAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Katibu Mkuu Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Florens Turuka akisalimia na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddy Kimanta
mara  baada ya kuwasili katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Mondoli(TMA) kwa ajili ya uzinduzi wa shahada ya kwanza ya mafunzo ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo leo(Picha na Pamela Mollel Arusha)

  Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania Jenerali Vanance Mabeyo  akisalimiana na Kaimu Mkuu wa  chuo cha uhasibu Arusha Dokt Faraji Kasidi, katikati ni Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao 

Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Florens Turuka akisalimia Generali Maj Othaman
mara  ya kuwasili katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Mondoli(TMA) kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo


Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka akisalimiana na Dr. Adolf B. Rutayuga ambaye ni kaimu mtendaji mkuu wa NACTE.

Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka akizungumza katika uzinduzi wa  uzinduzi wa shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo


Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akitoa hotuba fupi katika halfa ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo


 Meja jenerali Paul Peter Masao ambaye ni mkuu wa chuo cha mafunzo ya maafisa wanafunzi jeshi la ulinzi la Tanzania(TMA).

 Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha uhasibu Arusha Bi.Rukia Adam akisoma maelezo mafupi  juu ya uzinduzi wa wafunzo ya shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA). 


Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo  alisema mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia.
 

kushoto aliyevalia suti ni Profesa Johannes Monyoambaye aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha(IAA)
 Wanafunzi  wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo leo
Maafisa wa jeshi wakitumbuiza wata wa uzinduzi wa wafunzo ya sayansi ya kijeshi.
 Picha ya pamoja


Na Pamela Mollel,Monduli

Katibu Mkuu wa wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dokta Florens Turuka amesema kuwa jeshi hilo hivi sasa limejipanga katika kukabiliana na changamoto za ulinzi na usalama kwa kuwapatia askari wake mafunzo maalumu ya sayansi ya kijeshi. 

Aliyasema hayo Jana wakati akizungumza katika uzinduzi wa shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA). 

Alisema kuwa, kumekuwepo na matishio mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza Kwa namna tofauti ambapo hivi sasa matishio hayo yamegeuka na kuhamia kwenye mitandao, hivyo kama jeshi wana wajibu wa kujipanga zaidi kwa kuwaandaa maaskari ili waweze kukabiliana na hali hiyo mahali popote. 

Dokta Turuka alisema kuwa, wao Kama jeshi ni wajibu wao kujipanga mapema kwa kuangalia namna ya kuwajengea uwezo hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia ili kuboresha ulinzi na usalama hapa nchini. 

Kwa upande wa Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo alisema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo hayo kwa maaskari wake kulingana na mabadiliko ya kidunia hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia kwani ni eneo ambalo linahitaji elimu kubwa zaidi. 

Alisema kuwa, ni lazima wasonge mbele na kwenda na wakati kwani wasipofanya hivyo watabaki nyuma na kamwe hawataweza kukabiliana na vitisho vilivyopo  hivi sasa. 

Naye Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao alisema kuwa, wamekuwa wakitoa masomo ya kijeshi na kiraia ili kuwaandaa vijana katika hatua ya ngazi za  juu zaidi  kielimu  ambapo kwa kuanzia kozi hiyo watahiniwa  158  wataanza kozi hiyo mapema. 


Kwa upande wa Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi alisema kuwa, mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia ambayo yamekuwa yakileta manufaa makubwa Sana. 

Mwisho. 



No comments: