Social Icons

About us

Kwanza tunakushukuru sana kwa kuchukua muda wako na kufungua hii website ambayo imetengenezwa kwa malengo ya kukufikia wewe mwanachuo Mtanzania uliopo popote Duniani na wanavyuo wote walio maliza vyuo, Tumeamua kuanzisha hii website ikizingatiwa kuwa mpaka sasa Tanzania Kuna vyuo vingi sana na hakuna kitu ambacho kitatuunganisha, kwa kuanzisha website hii tunaamini kwamba itakua njia nzuri ya kuwafikia nyote naamini hata kama hamna mtandao wapa Kompyuta nyumbani Lakini mtazidi kuwa pamoja nasi kwa kupitia Internet Cafe na Labs za vyuo au kupitia simu yako ya kiganjani, Mtandao huu umegawanyika katika safu nyingi sana kama mnavyo ona hapo. tunawaombeni mpitie kila kona ya mtandao huu mpate kujua kila kipengele kina wataka kufanya nini, Tunaamini kwamba sisi kazi yetu ni kusimamia tuu mtandao huu lakini muongozaji ni wewe na nyie wanavyuo wote. na pia tunaamini kwamba Mtandao huu utakuwa na kumfikia kila mwanafunzi aliepo Tanzania na nje ya Tanzania, tumeona kuna  haja ta sisi wanafunzi kuungana na kuwa kitu kimoja. Tunaamini tunaweza kabisa ndio maana hatuja fungua page yoyote kwa Facebook wala sehemu yoyote ni hapa tuu, Kitu kingine cha msingi ambacho kimetufanya tuanzishe website hii ni swala zima la sisi wanavyuo ambao tunasoma bado kueleza mambo yetu mbali mbali hapa ikiwa ni matatizo yanavyo tukumba vyuoni,matukio ya Raha na Shida na taarifa mbali mbali za wanavyuo zote zitatumwa hapa. kwa ujumla tunaamini tutafika kwa ushirikiano wako wewe na nyie wanavyuo wote 
Asanteni sana,
Matukio na wanavyuo .