Social Icons

Wednesday 3 January 2018

BODI YA MIKOPO (HESLB) YAWAGEUKIA WAAJIRI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB) imesema kuanzia Jumatatu ijayo, Januari 8, 2018 itaanza kukagua taarifa za mishahara za waajiri (payroll) ili kubaini waajiri ambao wanawasilisha kiwango kidogo cha mikopo ya wafanyakazi wao ambao ni wanufaika pamoja na waajiri ambao hawawasilishi kabisa pesa hizo kwenye bodi hiyo kwa mujibu wa sheria ili wachukuliwe hatua stahiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema wanufaika wengi wa mikopo, wakiwemo wadaiwa sugu, wameonesha ushirikiano mkubwa katika kurejesha mikopo yao, hivyo kurahisisha kazi ya kukusanya madeni ya mikopo hiyo.

“Kiasi cha pesa za wadaiwa sugu kilichoiva na kinachotakiwa kuwasilishwa ni Tsh. bilioni 285, hii inajumuisha kuanzia kazi hii ya kukopesha ilipoanza.

“Tangu mwaka jana mpaka sasa tumewapata wadaiwa sugu 26,000, tunashukuru wanufaika hawa wamejitokeza na wanawasilisha mikopo yao. Kuna baadhi ya waajiri wanawasilisha vizuri marejesho ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, wengine hawasilishi na wengine wanawasilisha kiasi kidogo tofauti na asilimia 15 kama sheria inavyotamka.

“Kuanzia Jumatatu, Jan. 8, 2017 tutaanza kukagua taarifa kwenye payroll za waajiri wote waliosajiriwa kubaini waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa mikopo wanaodaiwa ili waweze kukatwa.

“Lengo la kufanya ukaguzi kwenye payroll za waajiri ni kubaini iwapo wana waajiriwa wanadaiwa na HESLB, waajiri wanaowasilisha kiwango kinachotakiwa, wanaowasilisha chini ya asilimia 15 na wanaokata pesa na hawaziwasilishi HESLB,” alisema Badru.

Hata hivyo, Badru amesema wamelazimika kufungua ofisi zao nchi nzima kwa ajili kusimamia malipo ya fedha hizo za mikopo, hasa wale waliotajwa kwenye orodha ya wadaiwa sugu ambapo wamewasambaza wakaguzi nchi nzima, kwa ajili ya kufuatilia waajiri wasiotekeleza wajibu wao wa kuwakata asilimia 15 wanufaika hao waliowaajiri.

No comments: