Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Jengo jipya la hosteli ya wasichana la Chuo cha
Madini Dodoma (MRI) ambalo ujenzi wake umekamilika hivi karibuni.
Bwalo la wanafunzi wa Chuo cha Madini Dodoma baada
ya kukarabatiwa na kupanuliwa.
Mkuu
wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (wa pili kutoka
kulia) akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa bwalo la wanafunzi. Wa
kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na
Madini, Caroline Musika akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo chaTehama, Wizara
ya Nishati na Madini, Francis Fungameza. Wa kwanza kulia ni Mshauri
Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd, Peter
Matinde.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika
akikabidhiwa funguo za jengo la hosteli la Chuo cha MRI na Mkandarasi
aliyejenga jengo hilo kutoka kampuni ya Chichi Engineering Construction
Ltd, Shaibu Katindi. Wanaoshuhudia ni Msanifu Majengo wa SMMRP, Arch.
Joseph Ringo (kulia), Mkuu wa Chuo cha MRI, Mhandisi Oforo Ngowi
(kushoto kwa Mkandarasi), Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na
washauri waliosimamia ujenzi wa jengo hilo.
Mkuu
wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (wa pili kutoka
kulia) akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa bwalo la wanafunzi. Wa
kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na
Madini, Caroline Musika akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo chaTehama, Wizara
ya Nishati na Madini, Francis Fungameza. Wa kwanza kulia ni Mshauri
Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd, Peter
Matinde.
Mkandarasi
kutoka kampuni ya Chichi Engineering Construction Ltd, Shaibu Katindi
(kulia) akielezea jambo kabla ya kuanza kwa ukaguzi wa jengo la hosteli.
Wengine katika picha ni wakaguzi pamoja na washauri waliosimamia ujenzi
wa jengo hilo.
Msanifu
Majengo wa SMMRP, Joseph Ringo (mwenye shati jeupe) akifafanua jambo
katika kikao na Mkuu wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi
(mbele katikati) mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Wa kwanza kushoto
ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis
Fungameza na kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Nishati na
Madini, Caroline Musika.
Mshauri
Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd,
Peter Matinde (kulia) akielezea jambo mara baada ya kufanyika kwa
ukaguzi wa jengo la hosteli la MRI. Sambamba nae ni Wataalamu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini na Mkandarasi.
Moja ya chumba cha jengo lililokabidhiwa la hosteli ya wasichana ya Chuo cha Madini (MRI) Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika
(kushoto) akiendelea na ukaguzi katika moja ya chumba katika jengo la
hosteli. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Wizara ya Nishati na
Madini, Francis Fungameza.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika
(kulia) akiwa sambamba na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Mkandarasi pamoja na baadhi ya washauri waliosimamia ujenzi
wakimsikiliza Mshauri Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM
Architects Ltd, Peter Matinde (hayupo pichani) wakati wa ukaguzi wa
jengo la hosteli.
JENGO LA HOSTELI CHUO CHA MADINI
LAKAMILIKA
Wizara
ya Nishati na Madini imepokea jengo la hosteli ya wasichana ya Chuo cha Madini
cha Dodoma (MRI) kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Chichi Engineering
Construction Limited katika makabidhiano yaliyofanywa hivi karibuni, mkoani
Dodoma mara baada ya ujenzi kukamilika.
Akizungumza
kwa niaba ya Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali
Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahya, wakati wa makabidhiano hayo Msanifu
Majengo (Architect) wa SMMRP, Joseph Ringo alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi
huo kutapunguza uhaba wa nafasi za malazi kwa wanafunzi hususan wa kike katika
chuo hicho.
Aidha,
alisema kulingana na takwimu za MRI inaonyesha kila mwaka usaili wa wanafunzi
unaongezeka na kwa kuwa chuo hicho hakina hosteli za kutosha, inawalazimu
wanafunzi wengi kupanga vyumba nje ya chuo jambo ambalo alisema si jema kwa
wanafunzi hao.
“Kila
mwaka wanafunzi wanaongezeka, kwahiyo kupitia jengo hili jipya la hosteli ya
wasichana nina imani changamoto ya malazi kwao itakuwa imetatuliwa,” alisema.
Katika
makabidhiano hayo, ilielezwa kuwa jengo hilo la hosteli linao uwezo wa kuchukua
jumla ya wanafunzi 88.Aidha,
mbali na jengo hilo la hosteli, makabidhiano hayo pia yalihusisha bwalo la
wanafunzi ambalo likikuwa limekarabatiwa kwa kupanulia pamoja na ofisi ya Mkuu
wa Chuo.
Ringo
alieleza kuwa, makabidhiano hayo yanakamilisha Awamu ya Kwanza ya Mradi wa
SMMRP kwa chuo hicho na kuongeza kuwa matarajio ya baadaye ni kujenga
miundombinu zaidi ili kukidhi mahitaji ya chuo hicho.“Mahitaji
ya chuo kuhusiana na majengo ni makubwa kuliko haya yaliyojengwa,” alisema.
Akizungumzia
mikakati ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mradi wa SMMRP (Additional
Financing), Msanifu Ringo alisema hatua zote za kuanza utekelezaji zimeanza.
“Matarajio
yetu ni kuwa malengo yaliyopangwa yatafikiwa kwa muda uliopangwa. Mradi huu
umebeba dhima kubwa ya kuhakikisha Watanzania wananufaika zaidi na sekta
ya Madini," alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo hicho cha Madini, Mhandisi Oforo Ngowi, alisema mradi
huo wa ukarabati na ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Chuo, bwalo la wanafunzi na
hosteli unao umuhimu wa kipekee katika kuboresha miundombinu pamoja na kuleta
maendeleo endelevu ya chuo hicho.
“Huu
ni ukombozi mkubwa sana kwa wanafunzi waliokuwa wanahangaika kutafuta malazi
nje ya chuo. Kilichobaki hapa ni kusoma tu”, alisema.
Mradi
huo wa Chuo cha Madini uliokabidhiwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya
usimamizi wa SMMRP na ulianza Julai, 2014 na kukamilika mwaka huu 2016 na ilielezwa
kwamba umegharimu takriban milioni 997.
Aidha
jengo hilo la hosteli limebuniwa na kampuni ya ubunifu Majengo ya PSM
Architects Ltd kwa kushirikiana na Howard Humphreys (T) Ltd na Mas-Q Associates
Ltd.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi zinazotekeleza miradi mbalimbali ya sekta ya madini chini
ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
No comments:
Post a Comment