Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Wanafunzi 204 wa Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine wapo hatarini kukwama kimasomo na kujikimu kimaisha baada ya
kukosa mkopo kwa muda mrefu tokea mwezi Novemba hadi sasa mwezi wa pili
2016.
Akizungumza
na waandishi wa habari chuoni hapo rais wa serikali ya wanafunzi wa
chuo hicho Osca Ndunguru ametupia lawama bodi ya mikopo kuendelea
kuwatesa wanafunzi huku wanafunzi hivyo amemuomba rais Magufuli
kutembelea bodi ya mikopo kuchunguza uozo unaofanyika na kwamba bodi
hiyo ihakikishe inashugulikia tatizo la wanafunzi hao ndani ya siku
tatu.
Nao
baadhi ya wanafunzi walioathiriwa na tatizo la kukosa mikopo wameeleza
kusikitishwa kwao na kwamba wanalazimika kuishi kwa tabu kwa kukopeshana
wanafunzi kwa wanafunzi wakitegemea bodi ya mikopo itawalipa fedha zao
lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hali ya maisha yao chuoni
yanazidi kuwa magumu.
Aidha
waziri mkuu wa serikali hiyo ya wanafunzi amesisitiza na kuiomba
serikali ya rais Magufuli kuangalia upya mfumo wa utendaji wa watumishi
wa bodi ya mikopo kwani wanafanya kazi hiyo kwa mazoea na upendeleo kwa
baadhi ya watu hali inayozorotesha maendeleo ya nchi.
No comments:
Post a Comment