Social Icons

Monday 15 February 2016

WANAVYUO IRINGA WAPONGEZA SIKU 100 ZA RAIS DR MAGUFULI WATAKA ATUMBUEMAJIPU NGAZI YA CHINI PIA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Katibu wa shirikisho la Vyuo vikuu CCM Mkoa wa Iringa Bi Mariam Fundi akikabidhi msaada kwa Yatima Kituo cha Faraja kata ya Nduli leo 
Katibu wa shirikisho la Vyuo vikuu la CCM Mkoa wa Iringa Mariam Fundi kushoto akikabidhi msaada kwa yatima
Aliyekuwa mgombea Urais katika mchakato wa ndani ya CCM kabla ya kumteua Dr John Magufuli , Bi Monica Mbega akisalimiana na kada wa CCM Kenan Kiongosi leo
Baadhi ya wanavyuo wanaounda shirikisho la Vyuo vikuu Mkoa wa Iringa wakiwa katika Picha ya pamoja na watoto Yatima wa Kituo cha Faraja kata ya Nduli leo
Na Matukiodaimablog

SHIRIKISHO la Vyuo vikuu la chama cha mapinduzi( CCM) Mkoa wa Iringa limepongeza kasi ya utumbuaji wa majipu inayofanywa na Rais Dr John Magufuli ndani ya siku 100 na kutaka kasi hiyo ya utumbuaji majibu ishuke ngazi za Mkoa na wilaya.

Tamko hilo la Shirikisho limetolewa na Katibu wa Shirikisho mkoani Iringa Bi Mariam Fundi leo  Mara baada ya kukabidhi misaada mbali mbali kwa watoto Yatima wa Kituo cha Faraja kata ya Nduli Wilaya ya Iringa kwa ajili ya siku ya wapendanao na maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM .

Fundi alisema kuwa shirikisho lake linaloundwa na Vyuo vikuu vitano vilivyopo mkoa wa Iringa , kuwa wamevutiwa na kasi ya utendaji Kazi wa Rais Dr Magufuli na hivyo kutaka baadhi ya wapinzani wanaobeza utendaji huo kumwacha Rais afanye kazi yake

"Sisi Kama wasomi wa Vyuo vikuu Iringa tumevutiwa sana na utendaji Kazi wa Rais wetu ..... Ombi letu zoezi la kutumbua majipu ishuke ngazi za chini zaidi nako huku kuna majipu yanayotesa wananchi"

Alisema kuwa utendaji wa Rais ndani ya siku 100 umeonyesha mwelekeo kwa serikali na hata kwa wananchi wa kawaida wanajivunia kuwa na Rais Mchapakazi 

Hata hivyo alisema utendaji huo Kazi wa Rais Dr Magufuli ili wananchi wa ngazi za chini pia waweze kuona matunda hakuna budi zoezi la utumbuaji majipu kwa wale wanaokwamisha maendeleo likawa endelevu kwa kutumbua majipu yaliyopo mikoani, Wilaya kata na vijiji.

Akielezea kuhusu siku ya wapendanao na misaada hiyo kwa Yatima walisema kuwa wao Kama wana Vyuo wameona kuihamasisha jamii kutoendekeza anasa wakati wa siku za wapendanao na badala yake kutumia siku Kama hiyo kusaidia Yatima ambao baadhi Yao walipoteza Wazazi kutokana na anasa za siku ya wapendanao.

Bi Fundi alitaja misaada hiyo kwa Yatima wa Kituo cha Faraja kuwa ni pamoja Vifaa vya shule, chakula , Sabuni na mafuta ya kupikia.

Huku Bw Kichima Kichima ambae ni Katibu wa itikadi CCM tawi la Chuo Kikuu cha Iringa mbali ya kupongeza Kazi nzuri ya Rais Dr Magufuli bado alitaka watendaji wa serikalini kujiongeza zaidi na kuacha kufanya Kazi kwa mazoea na kuwa lazima kila kiongozi kuonyesha utendaji wake na Kama akijibaini kuwa ni jipu Basi kujitumbua kabla ya kugonja kutumbuliwa.

Mwenyekiti wa shirikisho tawi la Chuo Kikuu cha Ruaha Bw Yusuph Rashid  katika siku 100 za Rais Dr Magufuli wamepata kushuhudia wanafunzi wa elimu ya juu ambao walikuwa wakisumbuka kupata mikopo Hivi sasa wamepata mikopo hiyo tena kwa asilimia nzuri zaidi .

Diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove pamoja na kuwashukuru wanavyuo hao kwa kujitoa kusaidia Kituo hicho cha Yatima katika kata yake bado amevutika na utendaji wa Rais ndani ya siku zake 100 za kuiongoza nchi

Diwani Mtove ambae ni mwenyekiti wa madiwani wa CCM jimbo la Iringa Mjini alisema kuwa amekuwa akiwajibika kutekeleza ilani ya CCM na kuwa mbali ya Rais kufanya Kazi kubwa kwa katika Taifa bado kwa upande wake ndani ya siku 100 ameanza mkakati wa Ujenzi wa Shule .
MWISHO






No comments: