Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega.
Na Mwandishi Wetu.
OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeanza kukagua taasisi za umma kuhusu utekelezaji wa matakwa ya sheria inayowataka kuwatambua waajiriwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu na kuwasilisha makato kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, sheria iliyoanzisha HESLB inazitaka taasisi zzote za umma kuijulisha Bodi kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya katika taasisi hizo ndani ya siku 28 na Bodi kuthibitisha kama waajiriwa hao ni wanufaika wa mikopo au hapana.
“Baada ya kuajiriwa mtu huyo ambaye amepata elimu yake ya chuo kikuu au taasisi yoyote ya elimu ya juu nadni au nje ya nchi kuanzia mwaka 1994 hadi sasa, mwajiri anapaswa kuitaarifu Bodi kwa maandishi ndani ya kipindi cha siku 28 tangu ajira hiyo,” inasomeka sehemu ya taarifa ya hiyo iliyochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari jana ikiwemo tovuti ya HESLB.
Taarifa hiyo, ambayo pia inapatikana katika tovuti ya HESLB, inaongeza kuwa baada ya Bodi kupokea taarifa kutoka kwa waajiri hao na kuthibitisha kuwa waajiriwa ni wanufaika wa mikopo, mwajiri atapaswa kuijulisha Bodi na kuanza kukata sehemu ya mshahara wa mwajiriwa ndani ya siku 30 na kuwasilisha makato hayo kwa Bodi ndani ya siku 15 kabla ya kila mwisho wa mwezi.
Kwa msingi huo, HESLB kupitia tangazo hilo, HESLB imewajulisha waajiri kuwa CAG amejumuisha matakwa hayop ya kisheria katika kazi zake za ukaguzi katika taasisi za umma kwa lengo la kuongeza kasi ya ukusanyaji mikopo iliyoiva.
“Ni imani ya HESLB kuwa waajiri katika utumishi wa umma watatoa ushirikiano kwa ofisi ya CAG ili kuondokana na matatizo ya kisheria,” amesema Bw. Nyatega katika taarifa yake.
HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili, pamoja na mambo mengine, kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa Tanzania wahitaji na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo tangu mwaka 1994.
No comments:
Post a Comment