Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Waziri
wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Fedha zilizo pelekwa katika
halmashauri zote hapa nchini kiasi cha shilingi bilioni 18.77 kwenye
akaunti za shule za msingi na Sekondari kwaajili ya kutoa elimu bure kwa
wanafuzi wa shule zote hapa nchini.
Gavana
wa Benki kuu ya Tanzania, Beno Nduru akifafanua jambo kwenye mkutano wa
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa
wizara ya Fedha na Mipango, Servacius Likwelile.
Kaimu
kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata
akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa
kila robo mwaka.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
KIASI
cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi
na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi
kusoma bure.
Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Pesa
hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na
Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na
bilioni 3 kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika
Halmashauri zote hapa nchini.
Dk.Mipango
amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa
Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa
matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.
Pia Waziri
wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote
za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi
matumizi ya fedha hizo katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila
mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.
Kwa hisani ya Michuzi Media Group
No comments:
Post a Comment