Na Anna Nkinda – Maelezo
Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaandaa mkakati wa kusafirisha wanafunzi kwa vitambulisho maalum vya wanafunzi kwa bei naafuu kwa kutumia mabasi ya UDA kwenda shule za pembezoni.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Kinondoni Omath Sanga wakati akisoma taarifa ya Idara ya Elimu kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipoitembelea shule ya Sekondari ya Kata ya Salma Kikwete iliyopo Kijitonyama wilayani humo.
Sanga alisema wanafunzi hao ambao wanatumia usafiri wa mabasi zaidi ya moja kwenda shule kwa siku kutoka majumbani kwao kuelekea maeneo ya Goba, Fahari, Kinzudi, Mabwe, Kisauke, Njechele, Mabibo, Malambamawili, Hondogo, Gogoni, Kibwegere na Kibweheri mara baada ya kukamilika kwa vitambulisho bivyo watalipa nauli ya shilingi 200 kwenda na 200 kurudi.
No comments:
Post a Comment