Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la polisi nchini, limewafukuza wanafunzi 212 wa uaskari katika
chuo cha taaluma ya polisi Moshi (MPA) kwa kosa kughushi vyeti vya
elimu ya sekondari.
Kamishina wa utawala na utumishi wa jeshi la polisi Thobias
Andengenye, aliyabainisha hayo jana wakati wa mkutano wa waandshi wa
habari pamoja na maafisa wa jeshi hilo katika ukumbi wa mkutano uliopo
katika chuo hicho, uliokuwa na lengo la kutoa taarifa ya wanafunzi wa
uaskari wanaoendelea na mafunzo ya awali chuoni hapo.
Alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na baraza la mitihani la
taifa walifanya zoezi la uhakiki wa vyeti vya wanafunzi hao na ndipo
ilipo bainika kuwa wanafunzi 212 kati ya wanafunzi 3,390 walighushi
vyeti vya elimu ya sekondari.
No comments:
Post a Comment