Bw. Stanley Bergman akiteta jambo na Balozi Manongi wanaonekana pia wageni waalikwa waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla hiyo.
Rais na Mwanzilishi wa MCW, Bw. Eddie Bergman akielezea historia ya
Taasisi hiyo ambayo aliianzisha ( 1999) akatumia fursa hiyo kutoa
shukrani zake kwa wadau , wafadhili na marafiki mbalimbali ambao
wameendelea kuiwezesha Taasisi hiyo na hatimaye kupitia kwayo kusaidia
jamii katika maeneo mbalimbali na uwezeshaji wa vijana.
Sehemu
ya wageni waalikwa, aliyekaa mstari wa mbele ni Bw. Ali Velshi ambaye
alikuwa ndiye mshereheshaji wa hafla hiyo. Bw. Velshi ni mtangazaji
maarufu wa vipindi vya Biashara katika Televisheni ya CNN hivi sasa
amehamia Al Jazeera Amerika
.Bw.
Stanley Bergman, Mwenyekiti na CEO, Henry Schein Inc akizungumza
wakati wa hafla ya miaka kumi ya uchangiaji wa Taasisi ya Miracle
Corners of the World ( MCW) ambayo pia imetimiza miaka kumi na tano ya
kuanzishwa kwake, katika mazungumzo yake alitoa shukrani na pongezi
kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa namna ambayo amekuwa akishirikiana na
Taasisi hiyo ambayo inaendesha shughuli hususani uboreshaji na
uimarishaji wa huduma ya afya ya kinywa.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akisema machache wakati wa hafla hiyo
Balozi
Manongi akiwa na Mwanamziki Maarufu Kanda Bongo Man, kutoka Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo, Kanda Bongo Man alikuwa mmoja wa wageni
waalikwa na kama alivyo Balozi Manongi naye pia ni Mwenyekiti wa Heshma
wa MCW
Na Mwandishi Maalum
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ameelezwa
kuwa ni kiongozi ambaye amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwa Taasisi zisizokuwa za
kiserikali na hivyo kuchagiza kasi ya taasisi hizo kuwekeza katika miradi ya kijamii nchini
Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa
na Bw. Stanley Bergman, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Henry Schein Inc, wakati wa hafla ya miaka
kumi ya uchangiaji wa shughuli
za Taasisi ya Miracle Corners of the World ( MCW) hafla
iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanziswa kwa Taasisi hiyo
yenye makazi yake Jijini New York,
nchini Marekani.
Hafla hiyo ilifanyika usiku wa Jumatatu na kuhudhuriwa
na wageni wa kada mbalimbali yakiwamo makampuni makubwa kama vile
NASDAQ OMX, CITI na the UPS Foundation ambayo
yamekuwa yakichangia shughuli za Taasisi hiyo.
Miongoni mwa wageni waalikwa alikuwa ni
Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
MCW ilianzishwa mwaka 1999 na Bw. Eddie Bergman ambaye wakati huo alikuwa na umri wa
miaka kumi na mitano, inajihusisha miradi ya kijamii ikiwamo ya huduma za afya, na uwezeshaji wa
vijana na kukuza ushirikiano na Taasisi
nyingine.
Taasisi hii
ilianza shughuli zake kwa kuanzisha kituo cha vijana
jijini Arusha na baadaye
ikasambaza huduma zake katika
mikoa ya Iringa, Dar es Salaam, Ruvuma na Zanzibar.
“ MCW inajivunia ushirikiano
na uhusiano wa karibu na Rais wa
Tanzania Mhe. Rais Jakaya Kikwete,
ambaye muwakilishi wake Balozi Manongi
yupo pamoja nasi usiku huu. Ni ushirikiano na
msaada wake wa hali na mali ndio unaoifanya MCW
iendele kutoa huduma zake nchini Tanzania. Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Rais Kikwete”. Akasema Bw.
Katika miaka yake
15 ya shughuli zake hususani uwezeshwaji wa vijana kutambua vipaji vyao vya uongozi na kubwa
zaidi uimarishaji na uboreshaji wa
huduma ya afya hususani afya ya
kinywa. MCW imekuwa ikishirikiana
kwa karibu sana na Chuo Kikuu cha Tiba na Sayasi (MUHAS) katika kuimarisha na
kuboresha Kitivo cha Meno kwa maana ya vifaa , mafunzo
na miundo mbinu.
Ni katika hafla hiyo, ambapo Rais na Mwanzilishi wa MCW, Bw.
Eddie Bergman wakati akielezea
mafanikio ya Taasisi hiyo alieleza kwamba kontena lililokuwa na vifaa vyenye thamani ya
dola za kimarekani 500.000 lilikuwa limewasili jijini Dar es Salaam
ambapo kwa ushirikiano kati ya
Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii na Bohari Kuu ya Madawa, ( MSD) kontena hilo
limeshatolewa bandarini na kukabidhiwa
Chuo Kuu cha MUHAS.
Dkt. Marion Bergman
ambaye ni Mkurugenzi wa miradi ya Afya katika MCW alishuhudia kuwasili kwa kontena hilo na makabidhiano.
Wakati wa hafla hiyo
ya jumatatu jumla ya dola za kimarekani
950,000 zilichangwa kwa madhumuni ya
kufanikisha shughuli za Taasisi hiyo
ambayo sasa inazihusisha pia Zambia,
Rwanda na Sierra Leone
Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Manongi, alieleza kwamba Tanzania imekuwa mmoja wa wanufaikaji wakubwa wa
MCW na kwamba Tanzania itaendelea kuenzi shughuli zake ambazo zimelenga katika kuinua
na kuimarisha huduma za afya katika
maeneo ya pembezoni mwa Tanzania.
No comments:
Post a Comment