Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwani Wema akitoa ufafanuzi kwa waandishi
wa habari (hawapo piuchani) kuhusu taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi
ya watu au makampuni binafsi kuhusiana na maudhui ya Tamko la Serikali lililoziagiza
wakala binafsi wa Huduma za Ajira kuwasilisha upya maombi ya usajili wa uwakala
kwa Kamishna wa Kazi.
Afisa Kazi wa
Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Themistocles Rumboyo akiwaeleza waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuwa hadi kufikia Februari mwaka huu jumla ya maombi
56 ya makampuni ya huduma za ajira nchini yamewasilishwa kwa Kamishna wa Kazi.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema.
Afisa Kazi wa
Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Omari Sama akijibu swali la waandishi wa habari
waliotaka kujua taratibu za kusajili wakala binafsi wa huduma za ajira hapa
nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema. PICHA ZOTE NA
FRANK MVUNGI- MAELEZO
No comments:
Post a Comment