Social Icons

Wednesday, 26 March 2014

Vyeti feki 1,035 vyakamatwa kwa waombaji wa kazi nchini

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sekretarieti ya Ajira,Riziki Abraham

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imekamata vyeti feki 1,035 (sawa na asilimia1.6) ya maombi ya kazi yaliyotumwa kwa miaka minne tangu kuanzishwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tangu wakati huo, jumla ya watu 65,000 walijitokeza na kuomba kazi katika sekretarieti hiyo.

Akizungumza na NIPASHE, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sekretarieti ya Ajira, Riziki Abraham, alisema katika kupokea maombi ya kazi, wamebaini udanganyifu wa hali juu wa vyeti kwa wanaomba kutoka makazini na wahitimu.


“Tangu miaka minne iliyopita hadi sasa, Sekretarieti ya Ajira imebaini kuwapo kwa matumizi ya vyeti feki wakati wa kuomba kazi, barua nyingi zimeonekana kuambatanishwa na nakala feki,” alisema.

Aliongeza: “Ni jambo la kusikitisha kuona mtu anatumia vyeti ambavyo si vyake kwa lengo la kujipatia kazi kiudanganyifu au wengine wanajaribu kuongeza vigezo ambavyo hana kwa kazi anayoomba ambapo husababishwa kutoitwa kwenye usaili,”, alisema.

Abraham alisema kuwa ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma inajipanga kutoa elimu kwa wahitimu na wadau mbalimbali wa elimu katika kuzitatua changamoto hizo.

Aliongeza kuwa sekretarieti hiyo katika kukabiliana na changamoto hizo wanatarajia kuhama katika mfumo wa analojia na kwenda dijitali ambapo wahitimu na walio makazini watatuma maombi kwa njia ya kielektroniki.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: