Social Icons

Friday 17 January 2014

WANACHUO wa Chuo kikuu cha St.Joseph Songea Wagoma‏


WANACHUO wa Chuo kikuu cha St,Joseph tawi la Songea wamegoma kuingia madarasani na kutoka kufanya shughuli za aina yeyote ndani ya chuo hicho huku wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali zikiwemo zilizoandikwa wamechoka kunyanyaswa na wakufunzi ambao wengi wao raia wa India baada ya uongozi wa serikali ya wanachuo kutimuliwa nyazifa zao na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita.

Kundi la waandishi wa habari wa mjini Songea mara tuu baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifika kwenye eneo la chuo kikuu cha St,Joseph kilichopo eneo la Luhuwiko mjini Songea ambako walishuhudia maandamano makubwa ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yaliyo ujumbe mbalimbali ikiwemo ya wamechoka kunyanyashwa na wakufunzi ambao ni wahindi.

Pia wanachuo hao walishuhudiwa wakiimba nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wamechoka kunyanyashwa kwani wao ni watu wazima hapaswi kulinganishwa na wanafunzi wa shule za msingi au sekondari huku wimbo mwingine ukiwa na ujumbe kama siyo mwalimu Nyerere kuleta amani wahindi msingefika kwetu kufanya biashara.

Kufuatia mgomo huo ililazimika askari polisi kufika kwenye eneo hilo huku wakiwa wamebeba silaha kwa lengo la kutuliza gasia ambao walitawanywa katika maeneo mbalimbali ya chuo lakini wanachuo waliendelea na maandamano yao huku wakiimba nyimbo za kushinikiza uongozi wa chuo uwarejeshe viongozi wa serikali ya wanachuo kwa sababu ya kutetea haki za wanachuo ambazo walizodai wahidi hao wamekuwa wakizikiuka.

Wanachuo hao ambao walidai kuwa malalamiko yao walishayafikisha kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakidai kuwa hali ya mazingira ya chuo hicho siyo manzuri lakini bado wahindi hao wameendelea na vitendo viovu licha ya mkuu wa mkoa kuwaangiza kuwa waache kuunyanyasa uongozi wa serikali ya chuo na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baad hi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.

Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baadhi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.

Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu 14 ambapo kati ya matundu hayo saba ya wanawake na saba ni wanaume wakati chuo hicho kinawachuo zaidi ya 1,200 na kufanya kusababisha tundu moja kutumiwa na wanachuo 64 badala ya kati 20 au 25.

Kwa upande wa viongozi wa serikali ya wanachuo waliyotimuliwa Aristides Munjwahuzi na waziri mkuu wake Deogratius Sanga waliwaambia waandishi wa habari kuwa matatizo makubwa yaliyopo ndani ya chuo hicho ni mengi ambayo wanachuo wakijaribu kulalamika kupitia uongozi wa serikali ya wanachuo badala yake uongozi wa chuo umefikia kuufukuza uongozi wa serikali ya chuo na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita jambo lilionekana kuwa ni uonevu mtupu.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa chuo hicho mtawa Antonia Emmanuel alisema kuwa suala la viongozi wa serikali ya wanafunzi la kuvuliwa madaraka na kusimamishwa masomo walishapewa maelekezo kuwa malalamiko yao walete kwa maandishi ili yajadiliwe lakini hawakufanya hivyo jambo ambalo aliliita kuwa ni dharau na badala yake ameshangazwa kuona wanachuo wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali lakini amesema tatizo hilo linahitaji kuwepo mazungumzo ya pande zote mbili yakiwa na lengo la kumaliza tatizo hilo. 

2 comments:

Anonymous said...

Sio siri wahindi wanyanyasaji sana wanatuona watanzania kama watumwa. Si songea tu kuna matatizo hata campus ya dar es salam matatizo kibao wamefunga vyoo eti maj hamna ukitaka kujisaidia mpaka uende mbali kupata huduma ya choo. Pia wanatabia ya kupiga wanafunzi. Eti unakuta umekosea kuandika jins alivyoelekeza anakupiga makofi na kutishia I will kill u. Cjui wakoje tunaomba serikali itusaidie wanafunzi. Ukichelewa kuingia darasan akakutangulia huruhusiwi kuingia darasan hadi amalize kipindi. Maan ya chuo ninini? Wanatuendesha kama watoto wa primary. Tunajuta kujiunga na st joseph.

Anonymous said...

Wanyanyasaji wahindi.