Social Icons

Sunday 26 January 2014

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII TENGERU


Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inaadhimisha miaka 50 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 27 Januari 2014 mpaka tarehe 31 Januari 2014.

Maadhimisho ya miaka 50 haya yataenda sanjari na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wizara utakaohusisha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa na Wilaya kutoka Tanzania nzima wanaofanya kazi katika Halmashauri zetu, Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Wadau wengine.


KAULI MBIU YA MAADHIMISHO YA MWAKA 2014 NI;

“Taaluma ya Maendeleo ya Jamii: Nyenzo Muhimu katika Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini wa Kaya”.

Vilevile kutakuwa na maonesho ya kazi za mikono, kutoka katika vikundi vya wanajamii wa Halmashauri za Arusha na Arumeru. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) watafanya maonyesho, pia watatoa huduma za afya kwa jamii.


Hivyo, wanakaribishwa wadau na wananchi wote kwa ujumla kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru.


IMETOLEWA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO KWA HISANI YA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA

No comments: