Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.
SHULE
ya Sekondari ya Loyola ya Jijini Dar es Salaam leo imeadhimisha Siku ya
Mtoto wa Kike shuleni hapo kwa kutoa semina mbalimbali kwa wanafunzi wa
kike juu ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike na namna ya
kukabiliana nazo hasa kwa wanafunzi shuleni. Mada anuai zimetolewa kwa
wanafunzi juu ya changamoto zinazowakabili hasa katika kipindi hiki
ambacho nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto ya utandawazi.
Miongoni mwa watoa mada waalikwa katika maadhimisho ya siku hiyo ni
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambao walitoa mada anuai kwa wanafunzi
juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili hasa kipindi hiki
ambacho wanahudhuria masomo yao.
Mgeni
rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia
Shauri akikata keki maalumu ya kuchangisha fedha zinazowasaidia baadhi
ya wanafunzi wanaokubwa na matatizo ambayo familia zao hushindwa
kuwasaidia .
Baadhi
ya wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha
pili suleni hapo walizawadiwa katika hafla hiyo. Mgeni rasmi wa na
Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akimpa
zawadi mmoja wa wanafunzi hao.
Mgeni
rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia
Shauri akilishwa keki na mmoja wa washiriki katika maadhimisho hayo.
Mgeni
rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia
Shauri (kulia) akilishwa keki na Mkufunzi Chuo cha Mafunzo ya Jinsia
(GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi wa Kidato cha Tano Loyola, wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kulishwa keki ya uchangishaji fedha kwenye hafla hiyo.
Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kulia akizungumza na vyombo vya habari kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.
Mo Blog
No comments:
Post a Comment