Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24),
amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni
hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo
lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D
kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel
Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya
Usimamizi wa Kodi akiwamwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika
katika chumba kinachotumiwa kulala nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi
wanapofika chuoni hapo kwa ajili yamasomo.
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa
kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuohiki, kwa hapa
chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi.
Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa funguo alikwenda kupumzika katika
chumba hicho na baadaye alikutwa amefariki huku mwili wake ukiwa umelala
kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi
napolisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi
Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu, Peter Alphonce, aliliambia
NIPASHE kuwa alikuwa na marehemu siku moja kabla ya kifo chake wakicheza
mpira na walimaliza kucheza vizuri na kuagana kuelekea hosteli.
“Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza mpira, hadi saa kumi tulipomaliza
aliniaga na kuelekea katika MachavaHostel ndiko anakolala,” alisema
Alphonce.
Credit:NIPASHE
No comments:
Post a Comment