Social Icons

Monday, 2 December 2013

DK KITILA AVULIWA UONGOZI CHUO KIKUU

Dar es Salaam, Tanzania. Taarifa zilizotufikia, zimeeleza kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umemvua madaraka kwa muda, Dk Kitila Mkumbo kuongoza Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE).LEO imefahamika kwamba Dk Kitila amevuliwa madaraka hayo kwa muda usiojulikana baada ya uongozi wa chuo hicho kupata taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa ni kiongozi wa Chadema huku akiwa mtumishi wa umma.


Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, ni kinyume cha sheria cha nchi mfanyakazi wa umma kuwa kiongozi katika chama cha siasa.
Kutokana na uamuzi wa chuo hicho wiki iliyopita Dk Kitila alipewa barua ya kusimamishwa.
Baada ya uamuzi huo Dk Kitila ataendelea kuwa mhadhiri mwandamizi kwenye kitivo hicho. 
Hivi karibuni Dk Kitila Mkumbo alivuliwa nafasi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kushiriki kuandika waraka wa badiliko ndani ya Chadema.

No comments: