Social Icons

Monday 2 December 2013

Rais Dr. Jakaya Kikwete ampongeza Mwanafunzi wa Shule ya Kata aliyeshinda Tuzo ya EAC



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi Peter Robert Kilave wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari ya Kata Tushikamane ya mjini Morogoro baada kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la Insha kuhusu Ujenzi wa Miundombinu Afrika Mashariki.Mwanafunzi Peter amechukua ushindi wa kwanza kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wan chi tano za jumuiya ya Afrika Mashariki .
Peter alipokea tuzo hiyo wakati wa Mkutano wa wa kuu wan chi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Speke’s Bay Resort,Munyonyo, Kampala Uganda juzi.Kutokana na ushindi huo Mwanafunzi huyo amepewa tuzo ya dola za Marekani 1500, na cheti na alikabidhiwa zawadi hizo na mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Picha na Freddy Maro




No comments: