Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kimewafukuza wanafunzi 43 na wengine Tisa kusimamishwa kuendelea na masomo kwa muda wa miezi Tisa kutokana na utovu wa nidhamu uliokithiri.
Kwa mujibu wa taarifa za Radio Uhuru Fm zinadai kuwa Pia Chuo hicho Kikuu kinawasiliana na Tume ya Vyuo Vikuu-TCU kuhakikisha kuwa wanafunzi hao hawatapewa nafasi ya kujiunga na Chuo chochote cha Umma sanjari na kutopatiwa mikopo na serikali kwa ajili ya kugharamia masomo yao.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa RWEKAZA MUKANDALA amesema hatua hiyo imefikiwa kufuatia vurugu zilizofanywa na wanafunzi hao kuanzia Desemba 12 na 13.
Inadaiwa kuwa wanafunzi hao wamefanya uharibifu wa mali uvunjifu wa amani pamoja na kujeruhi wanafunzi wenzao kutokana kuwapiga wakiwashinikiza kushirikiana nao katika vurugu hizo.
Chuo Kikuu cha Dar es salaam pia kimechukua hatua za kuimarisha ulinzi katika maeneo muhimu ya Chuo ili wanafunzi wengine waendelee kusoma bila kusumbuliwa sanjari na wafanyakazi wa chuo hicho kuendelea na majukumu yao ya kawaida ya kila siku.
2 comments:
Chuo kikuu cha mlimani - migomo kwanza. Masomo baadaye.
chuo kikuu dar wanatakiwa watatue chanzo cha migomo na wasikilize hoja za wanafunzi zina mantiki ndani yake waache ubabe kwa kuwafukuza wanafunzi, madaraka ni dhamana watumie nafasi walizopewa kutatua hoja za wanajamii
Post a Comment