Social Icons

Saturday 24 December 2011

Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Ashiriki Mahafali Ya Saba Ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)Nakumtunuku Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Chuo Kikuu Cha Taifa SUZA Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo hicho hawapo pichani kabla ya kuwatunuku shahada zao katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed Shein,akimtunuku shahada ya uzamivu ya heshima ya chuo kikuu cha Taifa SUZA Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume,wakati wa sherehe za mahafali ya 7 ya chuo hicho katika viwanja vya Mnazi mmoja Mjini Unguja leo
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA wakisubiri kutunukiwa Shahada zao na Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wa katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SUZA pamoja na wahitimu wa Chuo ngazi ya Stashahada baada ya kuwatunuku Stashahada zao katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhna Othman IKulu-Zanzibar


No comments: