Social Icons

Sunday, 11 December 2011

Vurugu lazuka katika Mahafali ya Tano ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki Muhimbili (MUHAS) hapo jana






Wakuu
wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili
(MUHAS) wakiingia kwa maandamano kwenye Mahafali ya Tano ya Chuo hicho
kabla ya kuzuka kwa vurugu.


Baadhi ya Wahitimu wa Chuo hicho wakiwa tayari kwa kutunukiwa nishani zao kabla ya kuzuka kwa vurugu.

Wanafunzi
wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili
(MUHAS) wakimsikiliza mwenzao kabla ya kusambalatishwa na kikosi kazi
cha Jeshi la Polisi (FFU).

Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mh. Ali Hassan Mwinyi (katikati) akiongozana
na baadhi ya wakuu wa Chuo hicho mara baada ya kuzuka kwa vurugu za
wanafunzi wa chuo hicho waliokiwa wakitaka kurudishwa kwa Serikali ya
Wanafunzi ambayo ilivunjwa hapo awali.

Ras Makunja akiwa na Gitaa lake tayari kwa kuendeleza muziki.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho akiwa ametiwa mbaroni na kina Ras Makunja.
wazee wakiwa tayari kwa lolote

Na Francis Dande

Wanafunzi
wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS), leo
wamesababisha shughuli za Mahafali ya Tano ya Chuo hicho kusimama kwa
muda baada ya kuzuka kwa fujo kubwa zilizopelekea Askari wa Jeshi la
Polisi kutumia mabomu ya kishindo ili kuwatawanya.

Wanafunzi
hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana huku wakiwa na
mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa
chuo hicho kurudisha serikali ya wanafunzi (MUHASSO).


Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo hicho, Deogratias Ntukumazina alitoa ahadi kwa
wanafunzi hao ya kuirudisha Serikali ya Wanafunzi pindi watakapofuta
kesi waliyofungua Mahakama Kuu kauli ambayo ilipingwa vikali na
wanafunzi hao na kutishia kuvuruga shughuli za mahafali zilizokuwa
zimesimama kwa muda kutokana na wanafunzi hao kufanya mkutano wao
uongozi wa Chuo mbele ya Jukwaa ambalo sherehe za kuwatunuku wahitimu
zingefanyika kutokana na kugoma kuondoka mahali hapo hata baada ya
uongozi wa Chuo kuwataka kufanya hivyo jambo ambalo lilisababisha Jeshi
la Polisi kuongeza nguvu ili kuwatawanya.


Hali
ilivyokuwa mbaya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile
alitoa amri kwa Polisi waliokuwa wakilinda Usalama kutumia nguvu jambo
ambalo lilisababisha baadhi ya wazazi waliofika katika mahafali hayo
kukimbia ovyo na kuanguka na watoto na kusababisha baadhi yao kuumia
kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na wanafunzi na baadhi ya viti
kuvunjwa na wanafunzi hao, katika kurupushani hiyo baadhi ya wanafunzi
walikamatwa na Polisi.
Katika
Mahafali hayo ambayo baadaye yalifanyika chini ya ulinzi mkali baada ya
polisi kuwatawanya wanafunzi hao baada ya njia ya majadiliano
kushindikana kutokana na jazba za wanafunzi hao waliokuwa walikuwa
wakidai serikali ya wanafunzi ilirudishwe jana
Hata
hivyo Kwa mujibu wa mmoja wa wanafunzi hao aliyetambulika kwa jina la
Njechele Boniface alisema kuwa walianza kukusanyika chuoni hapo majira
ya saa mbili asubuhi ili kufanya mkutano wao na Mwenyekiti wa Baraza la
Chuo, Deogratias Ntukumazina ili kuepuka kuingiliana na shughuli za
mahafali hayo lakini Mwenyekiti wa Baraza la Chuo alifika chuoni hapo
majira ya saa sita mchana na kusababisha kuingiliana kwa mkutano huo na
shughuli za mahafali hayo.Habari Kwa Hisani Ya Michuzi Blogu

No comments: