Social Icons

Monday 3 October 2011

MHE.BALOZI JUMA MWAPACHU ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA DODOMA



Mhe.Dkt.Jakaya MrishoKikwete, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania amemteua Balozi Juma Mwapachu  (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma kuanzia tarehe 14 Septemba 2011. Atakuwa kwenye nafasihiyokwakipindi cha miaka minne (4)

Balozi Mwapachu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Mohamed Ghalib Bilal ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kwanza na sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe.Balozi Juma Mwapachu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ikijumuisha nchi za Uhispania, Ureno, Tunisia, Morocco na Algeria.  

Balozi Juma Mwapachu amekuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali hapa nchini na amewahi kushika nyadhifa za juu katikaTaasisi za Umma na binafsi. Kwa muda mrefu alikuwa naibu Mwenyekiti wabaraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mhe.Balozi Juma Mwapach uamehitimu shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na alikuwa Mtanzania wa kwanza mwenye shahada ya Chuo Kikuu kujiunga na Jeshi la Polisi nchini.

Mhe.BaloziJuma Mwapachu aliwahi kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amewahi kuhariri na kuchapisha majarida na vitabu mbalimbali.

Uongozi wa Jumuiya nzima ya  Chuo Kikuu cha Dodoma inamkaribisha na kumtakia kila la kheri Balozi Juma Mwapachu katika majukumu yake mapya.
       
 IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
UNIVERSITY OF DODOMA
3 OKTOBA 2011

No comments: