Social Icons

Thursday, 29 September 2011

Vyuo Visivyokidhi Vigezo Kufungwa


                                 BAADHI YA WASHIRIKI WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI NA PICHA YA NNE NI MGENI RASMI AKIFUNGUA MKUTANO HUO.
                                 Na Elisante John, Singida
Septemba 28,2011.
WIZARA ya afya na ustawi wa jamii kwa kushirikiana na baraza la wauguzi,imeahidi kuvifunga vyuo vya afya visivyosajiliwa, ili kulinda ubora wa kiwango cha utoaji wa huduma ya afya nchini.
Hayo yameelezwa leo mjini hapa na waziri wa afya na maendeleo ya jamii Hadji Mponda,katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na muuguzi mkuu wa serikali Clavery Mpandana,kwenye mkutano mkuu wa 39 wa chama cha wauguzi nchini(TANNA).
Mponda alisema kuwa, vyuo hivyo vimekuwa vikitoa wataalamu wasiokidhi vigezo vilivyowekwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii, hali inayorudisha nyuma jitihada za serikali katika kuboresha huduma ya afya nchini.
Kutokana na hali hiyo, Mponda alisema serikali kwa kushirikiana na chama cha wakunga itavifungia vyuo hivyo, ili kulinda kiwango cha utoaji wa huduma za afya nchini.
Aidha kanali Mponda, pia amewataka wauguzi na waganga wakuu wa wilaya kuhakikisha wanafikisha fedha za vifaa kwenye vituo vya kutolea tiba, zitumike kwa kazi iliyokusudiwa.
Kwa upande wake Rais wa chama hicho kanali Ntuly Mwambingu ameiomba serikali kurejesha mfumo wa elimu wa zamani vyuoni, ili kusomea taaluma ya uuguzi iwe miaka minne, badala ya miwili inayotumika sasa.
Awali, ombi hilo lilitolewa na chama cha TANNA, katika mkutano huo unaohudhuriwa na wauguzi zaidi ya 700 kutoka mikoa yote nchini, na wageni mbalimbali kutoka mataifa ya jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADEC).
Hata hivyo baadhi ya wauguzi wameiomba serikali kuzikabili kikamilifu changamoto mbalimbali zinawazowakabili wauguzi,ili kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya afya.
Walisema ni vyema zaidi serikali ikayatatua matatizo yao kwa uwazi na ukweli, badala ya kuwataka wauguzi watumie akili zao katika kukabiliana nayo, hali inayoweza kuchochea vitendo vya rushwa kwa wanaowahudumia.


No comments: