Social Icons

Featured Posts

Tuesday, 24 November 2015

Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia elimu wanayoipata kuendesha maisha yao ili waweze kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia elimu wanayoipata kuendesha maisha yao ili waweze kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Prof. Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kituo cha Studi za Mawasiliano Martha Qorro ambaye alikuwa Mgeni Mashuhuri wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaaam.

Prof. Qorro alisema kuwa mwamko wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kujiunga na elimu ya juu nchini ni mzuri licha ya changamoto zinazowakumba wanafunzi hao wanapokuwa chuoni.

“Hawa ni wanafunzi wenye uelewa mzuri wakipata mahitaji yao ya lazima yakiwemo fimbo nyeupe, vifaa vya kuandikia kwa kutumia nukta nundu, baiskeli za miguu mitatu, viti maalu na mahitaji mengine ya kijamii” alisema Prof.Qorro.

Prof.Qorro aliongeza kuwa ni wajibu wa vyuo vikuu nchini kikiwepo Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kuwasisitiza kwa kuwauliza wanafunzi wanapojaza fomu za kujiunga waoneshe kuwa wanamahitaji maalum ili waandaliwe mahitaji hayo ikiwemo usafiri wa bajaji ndani ya chuo ili kuwawezesha kuwahi vipindi vyao katika maeneo mbalimbali ndani ya chuo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisye alipokuwa akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio chuo wakati wa Mahafali hayo alisema kuwa chuo hicho kimetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ambapo hadi sasa wamehitimu wanafunzi zaidi ya 8000 na jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu katika mahafali hiyo ya nane.

Naye muhitim wa mwaka wa tatu katika ngazi ya shahada ya ualimu katika masomo ya sanaa Andrea Sanga ambaye pia ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalum (mlemavu asiyeona) alisema kuwa mafanikio yake katika masomo yametokana na kuheshimu ratiba kuu ya masomo chuoni hapo pamoja na ratiba yake binafsi ya kujisomea.

Zaidi ya hayo, Sanga alisema kuwa maktaba ya chuo, ushirikiano mzuri kati yake na wanafunzi wenzake na walimu wake, kuhudhuria semina na kufanya kazi kwa wakati na kupunguza msongamano wa kazi nyingine ndiyo vimekuwa dira yake kuu ya mafanikio.

Sunday, 22 November 2015

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU ANOGESHA MAHAFALI YA 10 YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE DAR ES SALAAM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe akihutubia kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila akielezea mafanikio ya chuo.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, mwanafunzi, Benard Nyoni, aliyefanya vizuri katika masomo yake wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila na  Kaimu Mwenyekiti ya Bodi ya chuo, Evelyne Makalla.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, mwanafunzi, Godfrey Nchimbi aliyefanya vizuri katika masomo yake wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila, Kaimu Mwenyekiti ya Bodi ya chuo, Evelyne Makalla na Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MASO), Elias Kumanya. 
 Wahitimu wa ngazi ya cheti, stashahada na shahada ya kwanza waliofanya vizuri katika masomo yao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)
 Meza kuu ilivyokuwa ikionekana kwenye mahafali hayo.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto),  na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya chuo, Evelyne Makalla katika mahafali hayo.
   Brass Bendi ya Magereza ikiongoza maandamano wakati wa mahafali hayo.
 Mgeni rasmi na viongozi wengine wakiongoza maandamano kuelekea eneo la sherehe.
 Wahitimu wa ngazi ya cheti, stashahada na shahada ya kwanza wakiwa katika sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), yaliyofanyika Dar es Salaam.
 Wanafunzi wenzao wakiwapongeza watangulizi wao kwa kuhitimu.
 Brass Bendi ya Magereza ikitoa burudani katika mahafali hayo.
 Wahadhiri wa chuo hicho wakiwa katika mahafali hayo.
 Wageni waalikwa wakijumuika katika sherehe hiyo.
 Hapa ni kazi tu
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu waliofanya vizuri masomo yao wakiwa katika icha ya pamoja na meza kuu.
 Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.

Thursday, 19 November 2015

MUHIMU SANA: BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YATOA MAJINA YA AWAMU YA NNE NA YA MWISHO YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya AWAMU YA NNE NA YA MWISHO yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 718 waliopangiwa mikopo.

Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote nne yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.

MAHAFALI YA 45 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM‏

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

 Brass Band ikiongoza msafara wa maandamano ya Mahafali ya 45 ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
 Maprofesa na Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika Maandamano ya Mahafali ya 45 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru.
 Wananchi wakipata matukio wakati msafara wa Maandamano ya wahitimu walipokuwa wakipita mbele yao.

Saturday, 31 October 2015

MPYA KABISA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

PSLE-2015 EXAMINATION RESULTS

CHANZO NECTA

Tuesday, 27 October 2015

RAIS KIKWETE AKABIDHI VITABU CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA(NATIONAL DEFENCE COLLEGE)

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange vitabu kwaajili ya Chuo Cha ulinzi cha Taifa National Defence College(NDC) katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,Mkuu wa Chuo Cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakiangali baadhi ya vitabu ambavyo Rais ameviakbidhi kwaajili ya matumizi ya Chuo hicho.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(watatu kushoto),Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi Cha Taifa(NDC) Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukabidhi vitabu kwaajili ya National Defence College) katika hafla iliyofanyika ikulu jijijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Freddy MRO) 

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatatu Oktoba 26, 2015, amelikabidhi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vitabu kwa ajili ya vyuo vyake na maktaba zake, ikiwa ni mara ya tano kwa Rais Kikwete kulikabidhi Jeshi hilo vitabu wakati wa uongozi wake.

Vitabu hivyo 384 vilivyokabidhiwa leo vitatumiwa na Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha National Defence College (NDC) na wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho chenye hadhi ya kimataifa.

Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amehudhuria sherehe ya makabidhiano ya vitabu hivyo ambavyo Rais Kikwete amevikabidhi kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Hiyo ni mara tano kwa Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu kukabidhi vitabu kwa JWTZ katika azma yake ya kuboresha vyuo na maktaba ya vyuo hivyo vya Jeshi. Mpaka sasa, Rais Kikwete amekwisha kabidhi vitabu 3,136 kwa Jeshi.

Rais Kikwete aliahidi kulinunulia na kulikabidhi Jeshi vitabu (titles) mbali mbali 503 na kufuatia makabidhiano ya leo, sasa vimebakia vitabu (titles) 27 ambavyo navyo tayari vimenunuliwa na vinasubiriwa kusafirishwa kuletwa nchini kutoka vilikonunuliwa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2015

Tuesday, 13 October 2015

WANAFUNZI NA WALIMU BORA WA MASOMO YA SAYANSI WANEEMEKA NA NMB

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
1
Meneja Mwandamizi wa Benki Upande wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria (kushoto) akimkabidhi Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawii wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando (kulia) tuzo ya mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya wanafunzi nane na walimu wanne bora wa masomo ya biolojia na kemia.
2
Meneja Mwandamizi wa Benki Upande wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne na sita katika hafla ya utoaji tuzo.
3
Afisa Mauzo wa NMB, Joseph Mang’ongo akimuonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Aya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando kadi ya akaunti ya chapchap wakati wa maonesho yaliyokwepo katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa.
4
Wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa katika hafla ya kuwakabidhi tuzo kwa kuibuka vinara iliyofanyika mwishoni mwa wiki  katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
5Picha ya pamoja ya meza kuu, Uongozi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na wanafunzi na walimu katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne na sita jijini Dar es Salaam.
Katika kutambua jitihada za wanafunzi na walimu nchini, Benki ya NMB imewatunukia tuzo wanafunzi nane waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya biolojia na kemia kitaifa na walimu wanne waliowawezesha wanafunzi hao kuwa vinara katika masomo hayo tuzo ya jumla ya shilingi milioni 10  mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kila mwanafunzi aliefanya vizuri zaidi kwenye masomo hayo mawili amejishindia jumla ya shilingi milioni 1 na kila mwalimu shilingi laki 5.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Upande wa Taasisi - Noelina Kivaria alimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Bi.Kivaria aliwapongeza wanafunzi hao kwa jitihada zao shuleni na kuwaasa wanafunzi wengine wachukulie hiyo kuwa ni sehemu ya changamoto kwao hivyo wakaze kamba ili nao waweze kuwa vinara katika masomo yao.
Benki ya NMB imekuwa ikiipa sekta ya elimu nchini kipaumbele cha hali ya juu kwa kushirikiana na shule mbalimbali ndani na nje ya Dar es Salaam ikitoa misaada mbalimbali kama madawati.
Wanafunzi waliotunukiwa tuzo hizo ni:
 1. Samwel Felician-Nyamanoro Secondary School
 2. Jenipher Naali-St. Francis Secondary School
 3. Joshua Zumba-Uwata Secondary School
 4. Monica Mtei-Marian Girls Secondary School
 5. Felister Silvester-Ifunda Tech. School
 6. Mariam Mzingi-Feza Girls Secondary School
 7. Elisha Mmari-St. Mary Goreti Secondary School
 8. Innocent Yusufu-Feza Boys Secondary School
Walimu waliotunukiwa tuzo ni:
 1. Halima Tajiri-Feza Girls Secondary School
 2. Rogasian Fisso-Uwata Secondary School
 3. Grolius Rwabutomize-St. Mary Goreti Secondary School
 4. Jane Lalika-Marian Girls Secondary School


Monday, 5 October 2015

MAHAFALI YA SITA YA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI‏

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

PS1
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Dr Sr Hellen Bandiho akifungua rasmi kusanyiko la mahafali
..............................................................................
Wataalam wa Ununuzi na Ugavi nchini wameaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia miiko na maadili inayoongoza taaluma yao ili kuleta tija kwenye matumizi ya fedha za watanzania. Aidha Bodi imeagizwa kusimamia kwa ukaribu zaidi mienendo ya wanataaluma waliosajiliwa. Hayo yalisemwa na Dk. Hamis Mwinimvua Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akimwakilisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya Salum kwenye sherehe za mahafali ya sita ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB).
Aidha Bodi imepongezwa kwa kuzindua mtaala mpya wa masomo utakaonza kufundishwa kuanzia Januari 2016 na kutahiniwa mwezi Novemba 2016. “ni matumaini yangu pia kuwa mtaala huo utawajengea uwezo wataalam wote wa ununuzi na ugavi ili wazidi kuwa mahiri na wenye weledi mkubwa katika kufanya kazi zao” alisisitiza.
Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliipongeza Bodi kwa kuongeza masomo ya maadili, ujasiliamali, utafutaji wa masoko na usimamizi wa mikataba kwani eneo hili ni mahsusi katika kuleta maendeleo na tija katika matumizi ya rasilimali fedha. “ni matumaini yangu kwamba masomo haya yatakuza ajira kwani yatafungua wigo kwa wahitimu kuanza kujiajiri” alisema Mheshimiwa Waziri. Pia aliongeza kusema, serikali kwa upande wake imeboresha na itaendelea kuboresha zaidi mazingira ya ajira binafsi kwa minajili ya kuwawezesha wananchi kujipatia kipato halali cha kuendesha maisha yao.
Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliwaagiza waajiri wote kuhakikisha kwamba wanazingatia mahitaji ya sheria juzuu Na 179, inayowataka kuhakikisha kwamba wanaajiri watumishi waliosajiliwa na Bodi.
Alihitimisha kwa kuwapongeza wahitimu 494 walitunukukiwa vyeti katika ngazi za cheti cha awali, msingi na taaluma.
PS4
Mgeni Rasmi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi ya wahitimu katika picha ya pamoja
PS5
Sehemu ya wahitimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
PS3
Dk Hamis Mwinimvua akitoa hutuba kwa niaba ya mgeni rasmi
PS2
Dk Hamis Mwinimvua katikati aliyemuwakilisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Bodi, Dk Sr Hellen Bandiho na Mtendaji Mkuu Clemence Tesha wakimshuhudia Mgeni Rasmi akizidua mtaala mpya

Wednesday, 30 September 2015

IT BRIDGE YAWAFIKIA WANAFUNZI 60,000

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

IMG_3000
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na mwandishi wetu
JUMLA ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Hayo yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.

Alisema kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la awali la kwanza hadi la nne.

Aidha maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika kufanikisha mafunzo hayo.

Pia maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na kujifunza kwa gharama nafuu.

Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.
“Lengo la serikali kupitia Wizara ya Elimu ni kupanua wigo wa elimu hasa elimu ya awali kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo itabadilisha ufundishaji kutoka kutumia vitabu vilivyopo katika mfumo wa ‘hard copy’ na kuwa katika mfumo wa sauti na picha au ‘soft copy’,” alisema Profesa Bhalalusesa.
IMG_3089
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).

Alisema hadi kufikia wakati huu serikali imeshapiga hatua kubwa katika matumizi ya Tehama ambayo katika majaribio yake yameonesha kufanikiwa na wadau mbalimbali wa elimu wameyapongeza na kuyaunga mkono.

Profesa Bhalalusesa alisema kwa sasa wagunduzi mbalimbali wa mifumo ya Kompyuta inayoweza kutumika kufundishia ndio watakoonesha kazi zao na kutoa ufafanuzi wa kina kwa majaji wataochagua kazi chache na kuzifanyia majaribio kabla ya kuanza kutumika kufundishia.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mpango wa Kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kutoka Wizara ya Elimu, Agripina Habichi alisema mpango huo wa matumizi ya Tehama utasaidia wanafunzi kufahamu kusoma na kuandika kabla ya kuendelea na masomo ya darasa la tatu.

“Maonesho haya yanafanyika katika wakati muafaka ukizingatia tunataka kupiga hatua kubwa katika kuboresha elimu yetu. Washiriki wa maonesho haya wamekuja kutuonesha utawaalamu wao unaoweza kutumika kufundishia.

Lengo letu ni kuwafikia wanafunzi wengi zaidi ambapo tumeazimia kuzifikia shule zaidi ya 2000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 na hivyo tutakuwa katika kiwango bora zaidi cha utoaji wa elimu inayojitosheleza,” alisema Habichi.
IMG_3142
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kufundishia wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea yataimarisha kiwango cha elimu.

“Dunia imebadilika sana hasa katika sekta ya elimu na mawasiliano, hatuna budi kuendana nayo kwa kasi ileile ya ukuaji wake kwa kuimarisha mifumo yetu ya ufundishaji,” alisema Profesa Mchome.
Alisema wizara yake imeanzisha mpango maalum utakaosaidia wanafunzi kujifunza kwa njia ya kisasa ya kutumia mbinu za kielektroniki katika kujifunza na hivyo kuimarisha uelewa na kuongeza hamasa ya ufundishaji kwa wanafunzi.
Profesa Mchome alisema maonesho hayo yana lengo la kupata wadau mbalimbali waliobuni programu zinazoweza kutumika katika kufundishia kwa kutumia mifumo ya kielektroniki na hivyo watachaguliwa wachache wenye sifa na watakowezesha mafunzo hayo katika shule za Msingi na baadae katika ngazi ya sekondari.
IMG_3160
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
IMG_3161
Sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_3214
Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake katika kuendeleza sekta ya elimu nchini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kushoto) mara baada ya kuzindua maonesho hayo ambapo pia UNESCO inashiriki. Katikati ni Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa.
IMG_3217
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (katikati) akimsikiliza mmoja wa wadau wa elimu aliyetembelea banda la UNESCO kwenye maonesho ya TEHAMA yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo.
IMG_2982
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) akiwa na wadau wengine wa elimu wakipitia makbrasha mbalimbali katika mkutano huo.
IMG_3006
Pichani juu na chini ni baadhi wadau wa elimu waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.
IMG_3004
IMG_3028
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
IMG_3105
Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam yanakoendelea maonesho ya TEHAMA.