Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

Warembo
wa wanaowania taji la mrembo wa vyuo vikuu vya Tanzania “Miss Higher
Learning Institution 2017” wakiwa katika picha ya pamoja. Shindano hilo
lililopangwa kufanyika Septemba 29, limehairishwa mpaka mwishoni mwa
mwezi ujao.
Dar
es Salaam. Mashindano ya kumsaka mrembo wa vyuo vikuu vya Tanzania
“Miss Higher Learning Institution 2017” yaliyopangwa kufanyika kesho
Ijumaa ( Septemba 29) kwenye ukumbi wa King Solomoni, Namanga jijini
yamehairishwa.
Kuhairishwa
kwa mashindano hayo kumetokana na sababu za kalenda na waandaaji
kufikia makubaliano ya kusogeza mbele mpaka mwishoni mwa mwezi
ujao.Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya Glamour Bridal Tanzania
baada ya kupewa idhini ya waandaaji wa Miss Tanzania, Lino International
Agency kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).
Mkurugenzi
wa Glamour Bridal Tanzania Muba Saedo alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa
kwa lengo la kuboresha zaidi na hatua hiyo itawawezesha kufanya
mashindano yenye upinzani wa hali ya juu kutokana na idadi ya vyuo
mbalimbali vilivyothibitisha.
“Tumelazimika
kusogeza mbele mashindano kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo
wetu, warembo wataendelea na kambi chini ya mkufunzi wao Clara Michael
na ba matron, Blessing Ngowi,” alisema Saedo.
Mbali
ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), mashindano hayo yatashirikisha
vyuo vya Taasisi ya Uhasaibu Dar es Salaam (TIA), IFM, CBE, UDOM,
Tumaini – Makumira na Taasisi ya Uhasibu wa Arusha (IAA) na Chuo Kikuu
Cha Ardhi.
Saedo alivitaja vyuo vingine kuwa ni Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Tanzania Aviation University College na Magogoni.
No comments:
Post a Comment