TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa haitegemei kufutiwa
udahili kwa wanafunzi kwa baadhi ya vyuo, kutawakosesha baadhi ya
wanafunzi watarajiwa nafasi au kozi walizodhamiria kwenda kuzisoma.
Akizungumza kwenye Viwanja vya Maonesho, Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam jana, Ofisa Habari Mwandamizi, Edward Mkaku alisema TCU
haitahusika na wanafunzi ambao watakosa vyuo kwa sababu kwa sasa
wameratibu udahili na hivyo ni jukumu la mwanafunzi kutafuta chuo
kulingana na ufaulu alionao.
“Hatutarajii mwanafunzi kukosa chuo, na pia kufutiwa udahili kwa
baadhi ya vyuo siyo sababu ya wanafunzi kukosa nafasi kwenye vile vyuo
vilivyopo,” alisema.
CHANZOP HABARI LEO
No comments:
Post a Comment