Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza
namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za
Umoja wa Mataifa.
Vijana
kutoka Maeneo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mambo
mbalimbali yaliyokuwa yanazungumziwa wakati wa semina hiyo iliyofanyika
katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Kigamboni
Mwakilishi
wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Bw. Nelson akieleza
namna viongozi katika sekta mbalimbali wanavyoweza kusaidia kudumisha
amani katika Jamii.
Mshauri
wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi Bw. Anthony Luvanda akitoa
masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea
kwa kufanya shughuli mbalimbali.
Mwakilishi
kutoka Raleigh Bi. Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo
wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi
mbalimbali za Kiraia pia alielezea fursa zinazotokana na kujitolea
Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana
jinsi ya kupata 'Scholarship' zinazotolewa sehemu mbalimbali, na
kuwasihi kuwa wasikate tamaa kwa kuwa kuna nafasi nyingi za kusoma nje
ya nchi.
Bwana
Charles Ndiku akiwaelekeza vijana namna mbalimbali ambazo zinaweza
kuwasaidia kupata ajira,na aliwasisitiza ili waweze ishi kwa amani
yawapasa kuishi maisha bora ikiwa ni pamoja na kuwa na kipato endelevu.
Mwenyekiti
wa programu kutoka Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
salaam Bw. William Peter akieleza namna vijana wanavyoweza kubadili
mitazamo na kuwa na mawazo chanya ya maendeleo
Vijana mbalimbali wakichukua yale yaliyokuwa ya Muhimu
Vijana wakiwa wananyoosha mikono ishara ya kuonesha kuwa wameelewa vizuri kwa yale yote waliyoyasikiliza
Vijana wakiwa wanasikiliza kwa Makini.
Semina ikiendelea
Picha ya Pamoja
Picha zote na Fredy Njeje
"Kiongozi
bora ni pamoja na yule ambaye anahakikisha kuwa kuna amani katika eneo
la kazi na watu anaowaongoza" hayo yalisemwa na bwana Nelson aliyekuwa
mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Nchini
Tanzania wakati wa semina ya vijana katika kushiriki programu
mbalimbali za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana
na Global Peace Foundation Tanzania.
Alisema
kuwa kiongozi makini ni yule anayehakikisha kuwa kuna amani katika eneo
la kazi na kuwafanya wafanyakazi wake waishi kama familia moja ili
kuondoa migogoro mbalimbali ambayo inaweza ikazuirika.
"Amani
inatakiwa kudumishwa kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa
ujumla" alisema Nelson na kuongeza kukosekana kwa amani kunaweza
kusababisha maafa kama vifo kwa sababu ya vita pia uchumi kuyumba
kutokana na watu kuhofia kufanya shughuli za kimaendeleo kwa sababu ya
machafuko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa
program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa
uelewa ili wapate kujiunga.
Nae Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili
‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi
zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi
hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.
Mwisho Mshauri na mwezeshaji
katika mambo mbalimbali ya Bw. Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na
kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia
vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza
kutimiza malengo yao
Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya vijana 180, kutoka vyuo vikuu vya Mwalimu Nyerere,CBE, TIA, Bagamoyo, Kampala International University na St. Joseph, wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana wengine
Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya vijana 180, kutoka vyuo vikuu vya Mwalimu Nyerere,CBE, TIA, Bagamoyo, Kampala International University na St. Joseph, wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana wengine
No comments:
Post a Comment