Frank
Mvungi-MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar
es Salaam (DARUSO) kwa kusimamia vyema rasilimali za Taifa ili ziweze
kuwanufaisha watanzania wote.
Kauli hiyo imetolewa
leo Jijini Dar es Salaam na Rais wa (DARUSO)
Bw.John Jilili wakati wa mkutano wao na vyombo vya habari uliolenga kutoa tamko
la kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais kwa kuunda Tume iliyochunguza na kutoa
matokeo kuhusu mchanga (makinikia) unaosafirishwa nje ya nchi.
“Kuanzia sasa
uchakataji (processing) ufanyike hapa nchini na mikataba yote iwe na kipengele
kinachoyalazimisha makampuni yanayopewa leseni ya kuchimba madini kuwa na
mitambo ya kuchenjua makinikia ya madini yanayozalishwa na migodi hiyo.” alisema Jilili
Akifafanua zaidi Jilili amesema kuwa mikataba yote ya Madini
ni vyema ikatazamwa upya na kuzingatia maslahi mapana ya Taifa na si ya watu
wachache, kwani kwa kufanya hivyo kuonyesha dhamira ya dhati ya Serikali katika
kuleta mageuzi katika sekta ya madini nchini.
Katika mapendekezo yao DARUSO imebainisha kuwa Watanzania
wangependa kuona Mikataba na Sheria zilizopo zinaruhusu ukaguzi wa mara kwa
mara migodini ili Serikali ijiridhishe kuhusu kiwango cha madini
kinachozalishwa katika migodi hiyo pamoja na Serikali kuwa na ubia wa asilimia
50 au 49 na wawekezaji katika sekta ya madini.
Aidha Jilili alisema vyema pia kwa vyema kwa Viongozi wote
waliopewa dhamana ya kuwaletea wananchi maendeleo wakatekeleza wajibu huo kwa
uzalendo na kuepuka kuingia mikataba inayowezesha kuiletea hasara Serikali.
“Tunapenda kuwaomba watanzania wote wasomi na wasio wasomi
kumsaidia Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufikia lengo lake la kuleta
mageuzi makubwa ya kiuchumi na hayo yanawezekana tu kwa kuweka uzalendo mbele
na maslahi ya Taifa kwanza.” Alisisitiza Jilili
Aliongeza kuwa nidhamu na uwajibikaji katika sehemu za kazi
ni jambo la muhimu kwa Watendaji waliokabidhiwa majukumu ya kusimamia sekta
mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha
kuzaliwa kwa Tanzania mpya chini ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano.
“DARUSO inamthibitishia Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na
Watanzania wote kuwa iko sambamba nae katika harakati zake za kuikomboa nchi
yetu katika Nyanja zote ikemo kiuchumi” Alisisitiza Jilili
No comments:
Post a Comment