Na Lilian Lundo - MAELEZO
Mamlaka
ya Elimu Tanzania Tanzania (TEA) imetiliana saini na Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM) mkataba wa ujenzi wa uzio katika hosteli za Mwalimu
J.K. Nyerere Kampasi ya Mlimani.
Mradi
huo umedhaminiwa na TEA kupitia Mfuko wa Elimu (Education Fund)
utakaogharimu jumla ya shilingi 496,646,868 hadi kukamika kwa ujenzi
huo.
Mkataba
huo umesainiwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka
hiyo Graceana Shirima na Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Profesa Rwekaza
Mukandala wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kuwa utekelezaji mradi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Kwa
upande wake Prof. Mukandala aliwashukuru TEA kwa msaada huo na kuongeza
kuwa ujenzi wa uzio hizo ni suluhisho kubwa kwa wanafunzi watakaoishi
katika eneo la kampasi hiyo.
Alisema
kuwa uzio utasaidia kuimarisha usalama wa wanachuo na mali zao kutokana
na kuwepo eneo ambalo lina mzunguko mkubwa wa watu unaotokana na stendi
ya mabasi ya simu 2000 , maduka ya Mlimani City pamoja na viwanja hivyo
kutumika kama njia ya mkato na vijiwe kwa watu wasio na kazi.
TEA
tayari imefadhili miradi mbalimbali Chuo Kikuu cha UDSM ikiwemio ujenzi
wa vyumba vya mihadhara, ununuzu wa vitabu vya kiada, vifaa kwa ajili
ya wanafunzi kwenye mahitaji maalum, ufadhili wa kozi za "Pre Entry" kwa
wanafunzi wa like katika masomo ya sayansi, ununuzi wa mitambo na vifaa
vya Tehama.
Mwisho
No comments:
Post a Comment