Social Icons

Sunday 20 November 2016

GLOBAL PEACE FOUNDATION WATOA MAFUNZO JUU YA KUTATUA MIGOGORO NA KUDUMISHA AMANI YA NCHI SHULE YA SEKONDARI BENJAMINI MKAPA JIJINI DAR


 Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation nchini Tanzania Martha Nghambi akitoa maelezo mafupi kuhusiana na shirika hilo kuwa ni shirika ambalo halifungamani na imani ya dini yoyote, linalojengea watu ubunifu, maadili na kutoa mbinu mbalimbali za kutunza amani ambapo wanafanya kazi na mashirika ya umma pamoja na sekta binafsi pamoja na kulinda amani kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa UN Club katika shule ya Sekondari Benjamin Mkapa Joseph Malekela akitoa utangulizi na kuleleza kuwa mpaka sasa wana wanachama 130 na wanafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa na watanzania wote
Mmoja wa walimu akitoa utambulisho pamoja na kumkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation  Martha Nghambi 
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wanamsikiliza kwa Makini Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation nchini Tanzania Martha Nghambi(hayupo pichani) akitoa maelezo juu ya Shirika hilo.
Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation nchini Tanzania Martha Nghambi akitoa mafunzo ya ninamna gani ya kutatua migogoro katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na majumbani,mashuleni,mitaani pamoja na maeneo mengine mengi kwa lengo la kutunza amani
 Mwaafunzi wa Shule ya sekondari ya Temeke Aloyce Charles akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo

Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation  Martha Nghambi (wa pili kushoto)  akiandika Maswali ambayo anaulizwa na wanafunzi Mbalimbali
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa kidato cha Tano Grolia Michael akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo
Balozi wa Global Peace Foundation Tanzania akitoa elimu juu ya vijana na amani ambapo pamoja na yote alisisitiza vijana kujitambua ili kuweza kuendelea kudumisha amani.
Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation nchini Tanzania Martha Nghambi(wa kwanza kulia) akifuatilia jambo kwa makini wakati wa mafunzo hayo
Baadhi ya wanafunzi wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo
Mwenyekiti msaidizi wa Youth of United Nations Association (YUNA) Arafat  Bakir akielezea malengo endelevu 17 lakini akitilia mkazo zaidi lengo la 16 ambalo ni Amani, Haki na Taasisi Madhubuti aliwasisitiza vijana kuwa wanayonafasi kuhakikisha wanaitunza amani
Mafunzo yakiwa yanaendelea
Picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali
Picha ya pamoja na walioshiriki katika mafunzo mbalimbali

Picha zote na Fredy Njeje
Insta @fredynjejephotography
+255765056399

Katika kuhakikisha kuwa Amani inaendelea kudumishwa katika ngazi mbalimbali kuanzia familia mpaka jamii kwa ujumla Global Peace Foundation nchini Tanzania wameendelea kutoa elimu hiyo katika maeneo mbalimbali ambapo safari hii mafunzo hayo yametolewa katika Shule ya Sekondari ya Mkapa ambapo walijumuishwa wanafunzi kutoka shule mbalimbali kupata mafunzo hayo.

Akitoa mafunzo kwa wanafunzi hao Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation Nchini Tanzania Martha Nghambi  ya ninamna gani ya kutatua mizozo, migogorona migongano katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na majumbani,mashuleni,mitaani pamoja na maeneo mengine mengi kwa lengo la kutunza amani ambapo alieleza kuwa migongano huweza kutokea katika sehemu zaidi ya moja kama baina nchi na nchi, mtu na mtu au shirika kwa shirika ambapo yote hutokea baada ya makundi hayo kushindwa kufikia muafaka katika jambo,ambapo migongano hiyo huweza tokea majumbani, mashuleni pamoja na maeneo tofauti.

 Kutokana na hayo imeonekana kuwa nchi majirani zetu waliotuzunguka hawapo salama kutokana na viashiria hivi hivyo watanzania tuna kila sababu ya kuhakikisha kila mmoja anakuwa balozi mzuri wa amani na nchi haiwezi endelea endapo hakuna amani , hakuna maendeleo endelevu bila amani.

Aliezea kuwa migongano huweza kutokeakutokana  na tofauti za kidini,Siasa ambapo aliwasihi vijana kuwa kama wamejiingiza huko wajitahidi kutopenda mpaka kupitiliza ili kutunza amani,Imani mbalimbali na uwezo.  

Aliongeza kuwa sababu ambazo zinaweza kuchochea migogoro ni pamoja na kuto kuwasiliana vizuri baina ya watu,'extremist',Siasa na Dini , aliendelea kueleza kuwa matokeo ya migogoro hiyo ni pamoja na pande zote mbili kukosa kitu fulani,upande mmoja kushinda na mwengine kukosa na tatu ni pale ambapo kila mmoja ameshinda.


Alimalizia kwa kusema kuwa Dunia yote  watu wanahitaji amani na nijukumu letu sote kuhakikisha amani inaendelea kuwepo na kuelezea vidokezo ambavyo vinaweza kuendelea kudumisha amani ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wakati wote unatakiwa kufurahia maisha yako pia kumruhusu mwenzio kufurahia maisha hayo,kama unapenda kufanyiwa jambo basi nawe mfanyie mwenzako na kama haupendi kufanyiwa jambo basi usiruhusu kumfanyia mwenzako jambo hilo na kuhakikisha tunaendelea kusambaza upendo.

Nae Balozi mmoja wa mabalozi wa Global Peace Foundation Anna Mwalongo alitoa elimu juu ya vijana na kujitambua  ambapo aliwahimiza vijana wote kuwa wanajukumu la kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa kwa wao kujitambua kwa kufanya hivyo hakutakuwa na uvunjifu wa amani.

Pia akizungumza na wanafunzi Makamu Mwenyekiti wa YUNA Arafat Bakir alitoa elimu na maelezo juu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ambapo pamoja na kuyaelezea yote lakini alijikita katika lengo la 16 ambalo linaelezea juu ya Amani, Haki na Taasisi madhubuti , alisema kuwa swala la kutoa elimu juu ya kudumisha amani huwa haliishii mijini tuu lakini inawafikia mpaka watu wa pembezoni na kusisiza kuwa ni jukumu letu sote kuhakikisha amani inaendelea kutunzwa 

PIA WANAPATIKANA
Twitter@globalpeacetz 
Instagram @globalpeacefoundationtanzania
Facebook  @globalpeacefoundationtanzania
 

FAHAMU KUHUSU GLOBAL PEACE FOUNDATION

Global Peace Foundation yenye makao yake katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile.

Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka jana ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla. 

Mnamo mwezi wa saba mwaka 2015 Global peace foundation waliandaa Mkutano mkubwa wa amani uliofanyinka Zanzibar uliojulikana kwa jina la Global peace Leadership Conference (GPLC Zanzibar) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais Mh. Balozi Seif Ali na kuhudhuriwa zaidi ya watu 200 wakiwemo marais wastaafu kutoka nchi mbalimbali.

Global Peace Foundation kwa kushirikiana na Inter Religious Council For Peace walizindua kampeni ya kuhamasisha amani kipindi cha uchaguzi wa urais mwaka jana, kampeni iliyojulikana kwa jina la "Amani Kwanza" 

Kwa sasa Global Peace Foundation wana endeleza harakati za kuhamasisha amani kupitia kampeni yao ijulikanayo kama "Vijana Na Amani" ambapo imekuwa ikiwashirikisha kundi la vijana pamoja na makundi mengine ikiwemo wazazi na walezi. 

Mpaka sasa wameshaweza kufanya midahalo mbalimbali yenye lengo la kuhamasisha amani, pamoja na kutoa mafunzo mbalimbali juu ya umuhimu wa kutunza amani mashuleni, vyuoni pamoja na sehemu za makazi, na pia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

No comments: