Na:
Frank Shija, MAELEZO
14/11/2016
Bodi
ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kupewa notisi ya siku thelethini
(30) wawe wameanza kulipa madeni yao kabala hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi
yao.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB) Abdul – Razaq Badru
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari
MAELEZO kuhusiana na wadai sugu leo
Jijini Dar es Salaam.
Badru
amesema kuwa notisi hiyo inawalenga wanufaika wa waliokopeshwa na muda wa
mataraji ukapita bila wao kuwasilisha taarifa zao na kulipia madaeni ya mikopo
ya eleimu ya juu waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/95.
Alisema
kuwa jumla ya wanufaika 93,500 walinbainika na kupelekewa Ankara ya madeni yao
ili waweze kulipa hata hivyo kati yao ni
wadaiwa 81,055 ndiyo wanaendelea kulipa madeni yao.
Aidha
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wapo wadaiwa sugu takribani 142,470 wenye mikopo
yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 239 hawajajitokeza wala kuanaza
kulipa mikopo yao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Abdul Mussa amesema kuwa urejeshaji wa
mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 25 zimerejeshwa
hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.
Hatua
hii ya kutoa notisi ndani ya siku thelathini inafuatia kutokana na kuvunjwa kwa
sheria namba ya 19A (1) cha sheria za Bodi ya Mikopo Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo pamoja na hatua hiyo Bodi imeazimia
kuchukua hatua nyingi za ziada.
Hatua
hizo ni pamoja na kuyatangaza majina ya
wadaiwa sugu hadharani ili waajiri, wadhamini wao na wadau wengine wenye
taarifa za wasugu waziwasilishe,kuwasilisha majina ya wadaiwa kwenye taasisi
zinazotunza taarifa za ukopaji na kukamilisha taratibu za kuwafikisha
mahakamani kwa hatua za kisheria.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment