Mkuu
wa Chuo cha Ufundi VETA Eng, Lucius mwishoni mwa wiki akiongea na
baadhi ya walimu na wanafunzi VETA kuhusu mfumo wa masomo kwa njia ya
simu za mkononi wa VSOMO ambapo zaidi ya vijana 28 elfu
wamejiandikisha ili kusoma kwa mtandao wa VSOMO. Mkuu huyo pia amesema
ndani ya miezi miwili chuo chake kitaongeza kozi zingine 10 ili
wanafunzi wanaozipenda waanze kusoma.
Vijana zaidi ya 28 elfu wajitokeza kwa kujiandikisha VSOMO kuomba masomo ya VETA kwa njia ya simu
· Kozi nyingine za VETA 10 kuongezwa kwenye mfumo wa VSOMO ili kusomwa kwa simu
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel wakishirikiana na VETA wameanza kuona
mafanikio ya mfumo wa Masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kwa
njia ya simu za mkononi ujulikanao kama VSOMO ambapo tayari umefanikiwa
kupokea maombi na kuaandikisha vijana zaidi ya elfu ishirini na nane
kuomba kusoma kozi za VETA kwa njia ya simu za Airtel toka
ulipozindiliwa mwaka huu mwezi mei.
Akiongea
mwishoni mwa wiki wakati wa hafla fupi ya kueleza mafanikio ya mfumo wa
VSOMO iliyofanyika katika Ukumbi wa VETA kipawa Mkuu wa Chuo cha Ufundi
VETA Eng, Lucius Luteganya alisema “Airtel na VETA baada ya
kuanzisha mfumo wa VSOMO yaani masomo kwa njia ya simu za mkononi na
kupeleka taarifa katika vituo vya VETA vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,
Dodoma, Dar es salaam, Arusha na Mbeya, leo hii zaidi ya vijana 28
elfu wameshajiunga na mtandao wa VSOMO kwa lengo la kutaka kuanza
kusoma, hii inaonyesha kuwa mfumo huu wa kusoma kwa njia ya simu
umekubalika na pia kunauhitaji mkubwa wa vijana kutaka kusoma VETA”
Eng,
Lutejanya alisema kuwa “Kwa vijana wote ambao tayari wameshapakua
aplikesheni ya VSOMO katika simu zenu sasa ivi wanaweza kuchagua kozi na
kuanza kusoma papo hapo popote walipo mara tu baada ya kulipia, kozi
zilizopo sasa tayari kwa kusoma ni kozi ya Umeme wa nyumbani,
kuchomelea, ufundi wa pikipiki, maswala ya urembo, kutengeneza aluminum,
pamoja na ufundi simu”
“Baada
ya kuona ongezeko la vijana kujisajili na huduma hii ya VSOMO tayari
tumewasiliana na baadhi ya vijana kwa kushirikiana na mdhamini wa mradi
huu Airtel ili kubaini kozi wanazotaka, hivyo basi tumeshazijua na
tumejipanga ndani ya miezi miwili kuanzia sasa tutapandisha kozi zingine
10 kwenye mfumo wetu wa VSOMO ili vijana wote waliojiandikisha waweze
kuchangua kozi wanazotaka” alieleza Eng, Luteganya.
Mradi
wa VSOMO uko chini ya mradi wa kijamii wa Airtel FURSA ukiwa na lengo
la kuwasaidia vijana kuweza kujisomea kozi za ufundi stadi ili
kujipatia ajira za uhakika. Mradi wa VSOMO ulibuniwa kwa ushirikiano
kati Airtel na Mamlaka ya elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hivyo
kufanya simu ya mkononi kuwa Darasa.
No comments:
Post a Comment