Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255629914471. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi inatarajia
kuvifanyia uhakiki wa ubora ubora vyuo vyote, vinavyotoa shahada nchini
vya umma na vya binafsi kuanzia kesho.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Maimuna Tarishi, vyuo vyote
vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu, zitakazofika kwa
ajili ya kufanya uhakiki huo.
Aidha, Tarishi alisema katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi
wanaoendelea na masomo, vyuo vyote pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
(TCU), leo vitatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba
walidahiliwa kupitia TCU.
“Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti
ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na uongozi wa
TCU haraka iwezekanavyo ili kupata maelezo zaidi,” alisema Katibu Mkuu
huyo.
Alisisitiza kuwa mwanafunzi yeyote ambaye hatazingatia maagizo hayo ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.
Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, alitangaza kuanzisha msako wa
wanafunzi hewa vyuoni baada ya kubainika kuwepo kwa wanafunzi hewa
wanaopewa mikopo wakiwemo wengine wanaosoma shahada huku wakiwa hawana
sifa.
CHANZO GAZETI LA HABARI LEO
No comments:
Post a Comment