Social Icons

Tuesday, 4 October 2016

SHULE BORA YA MUZIKI TANZANIA ALPHABETA MUSIC CENTRE YAJA NA MPANGO BORA KWA WASANII WOTE NCHINI .

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255629914471. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
 Moja ya matukio ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu. Mkurugenzi wa ALPHABETA MUSIC CENTRE akikabidhi Cheti kwa moja ya wanafunzi huku aliekuwa  Mwakilishi wa BASATA Bw. Angelo Luhala akishuhudia.
 Dada Etheline mmoja wa wanafunzi waliopitia ALPHABETA MUSIC CENTRE akilicharaza gitaa kwa umahiri.
 Studio ya kisasa inayo milikiwa na Shule ya ALPHABETA MUSIC CENTRE.
 Wanafunzi wakiendelea na mazoezi ya vitendo.
 Mkurugenzi wa ALPHABETA MUSIC CENTRE Ndugu Mark Manji akionyesha umahiri wake akipuliza Tenor Sax.
Wanafunzi wa ALPHABETA MUSIC CENTRE wakiwa darasani.


Shule bora iliyo jikita katika kukuza vipaji na suala zima la sanaa ya muziki Tanzania, wameanzisha masomo  ya muziki juu ya matumizi ya Ala na vifaa mbalimbali vya muziki vya kisasa na vya utamaduni ili kukuza vipaji vya wasinii wa muziki nchini.

Akizungumza leo shuleni hapo Mkurugenzi wa ALPHABETA MUSIC CENTRE Ndugu Mark Manji, amesema shule  hiyo tangu kuanzishwa kwake kume kuwa na mwitikio  makubwa  kwa vijana na wasanii mbalimbali wadogo kwa wakubwa kwa kuamua  kwenda na wakati kwa kufanya muziki wa kisasa na wa kisomi.

 " Shule yetu ilianzisha mpango  wa  kufundisha masomo mbali mbali ya Ala na matumizi ya vifaa vyote vya kisasa na vya  kitamaduni na pia tuna studio ya kubwa na ya kisasa ili kukidhi malengo na tija kwa wasanii watakao pita ALPHABETA MUSIC CENTRE kwani elimu hiyo inatolewa kwa gharama nafuu sana ili kila Mtanzania anayehitaji elimu ya muziki  aweze kumudu " alisema Bw .Manji

Akifafanua  zaidi  Bw. Manji amesema wamekuwa wakifundisha masomo ya matumizi ya Ala na utumiaji wa vifaa mbalimbali vya muziki kama upigaji wa vyombo vya muziki kwa kutumia Nota pia tuna vifaa vingi kama Drums na Tumba, vifaa vya kupuliza kama Trumpets, Trombones na Saxophones, tunafundisha  kupiga keyboards, magitaa ya umeme na box, kutumia vifaa vya kitamaduni kama ngoma, marimba pia tunafundisha kuimba, kutunga nyimbo na tuna  studio kubwa nzuri yenye vifaa vya kisasa kwaajili ya kufundishia na kufanyia mazoezi ya vitendo kwa wanafunzi wetu wa ALPHABETA MUSIC CENTRE .

Ndugu Mark Manji  ame wasisitizi  vijana kwa wazee anaotaka kuingia kwenye sanaa na waliomo kwenye sanaa hii ya muziki kujiunga na shule hiyo ya muziki ya  ALPHABETA MUSIC CENTRE iliyopo Tabata Liwiti, Dar es salaam  kwani wao wanatoa elimu bora ya muziki. Pia amewataka wasanii wadogo kwa wakubwa kutumia Studio ya ALPHABETA kwani ni bora na ya kisasa ambayo ni moja ya studio bora yenye vifaa vya kisasa na  kwa gharama nafuu sana.

Shule ipo Tabata, Liwiti au wasiliana nasi kwa no 0754776640,  0784737216

MSANII ELIMU KWANZA

No comments: