Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira, akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi
ngazi ya juu na kuwatunuku Maafisa Magereza 98 Cheo cha Mrakibu
Msaidizi. Katika hotuba yake Katibu Mkuu aliwaasa wahitimu hao
wakaitumie taaluma walioipata chuoni hapo kwenda kuwahudumia Watanzania
kwa uadilifu. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa
Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja, akihutubia wakati wa
hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Wahitimu
98 wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja
vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Gwaride
la Maafisa Wahitimu wa kozi ya Uongozi ngazi ya Juu wa Jeshi la
Magereza likijiandaa kupita mbele ya Jukwaa la Mgeni kwa heshima kama
wanavyoonekana wakiwa wakakamavu katika picha. Sherehe za kufunga
Mafunzo hayo zimefanyika leo Juni 14, 2016 katika Viwanja vya Chuo cha
Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu kama inavyoonekana katika picha.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa
Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu aliyefanya vizuri katika masomo ya
Medani kwa niaba ya Wahitimu wote wa kozi hiyo(kulia) ni Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akishuhudia tukio hilo la
uvishaji cheo.
Maafisa
Wandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni Waalikwa kutoka Taasisi
mbalimbali wakifuatilia kwa karibu Gwaride la Wahitimu.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa
maelezo mafupi juu ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza kabla ya
kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya
Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kulia)
akimuongoza Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira kuelekea eneo la hafla ya kufunga rasmi
Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu wa Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, ACP. Erasmus
Kundy(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment