Social Icons

Monday, 8 February 2016

PSPF YAZIDI KUJITANUA, WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAZIDI KUMIMINIKA KWENYE MFUKO HUO KWA KUJIUNGA NA MPANGO WA PSS

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


 Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto, akitoa elimu juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSS, na umuhimu wa wanafunzi wa UDSM kujiunga na Mfuko huo kupitia Mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS. Warsha hiyo iliyokusanya wanafunzi karibu 3,000 ilifanyika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani jijini Dar es Salaam, Februari 6, 2016

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said


WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani na wale wa Chuo Kikuu Cha Tumaini, kampasi ya Dar es Salaam, (TUDACO) wameendelea kuchangamkia “fursa” kwa kujiunga na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, PSS


Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, UDSM, Kitapenda Ahadi na Makamu wake, Irine Deodatus Ishengoma, waliongoza mamia ya wanafunzi pale mlimani kwa kujaa fomu za kujiunga na Mfuko huo.

Hatua ya kujiunga na Mfuko huo ni baada ya semina iliyotolewa na Maafisa wa Mfuko huo, wakiongozwa na mabalozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Flaviana Matata, na Msanii maarufu wa hapa nchini, Mrisho Mpoto almaaruu kama “Mjomba”.

Akizungumzia huduma zitolewazo na Mfuko huo, Afisa wa Matekelezo (compliance), wa PSPF, Albert M.Feruzi na Hadji Jamadary, walisema, kuna uchangiaji wa mpango wa lazima, (mandatory scheme) na ule wa hiari Supplementary Scheme) na kuwataka wanafunzi hao ambao wengi wao ni wa mwaka wa mwisho, kuchangamkia fursa kwa kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari.

Nao mabalozi wa PSPF, waliwaeleza wanafunzi hao kuwa pindi wakijiunga na PSPF, hawatajutia uamuzi wao, kwani kuna watafaidika na mafao mbalimbali kama vile mkopo wa elimu, fao la uzazi, mkopo kwa muajiriwa mpya, mkopo wa nyumba na mkopo wa viwanja.

Chuo Kikuu ChaTumaini, tawi la Dar es Salaam, (TUDACO), ndio waliokuwa wakwanza kujiunga na Mfuko huo ikiwa ni wiki moja tu baada ya wanafunzi wenzao hapo hapo kuchukua uamuzi huo.

Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Rahma Ngassa, (wakwanza kushoto), mhamasishaji, Anthony Luvanda, (wapili kushoto), Mabalozi wa PSPF, Flaviana Matata, (watatu kushoto) na Mrisho Mpoto, (wane kushoto) na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Irine Deodatus Ishengoma, wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na uongoz wa DARUSO kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, na kufanyika ukumbi wa Nkuruma wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mamia ya wanachuo walijiunga na Mfuko huo kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS)

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, wakijaza fomu za kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wakati wa semina ya siku moja iliyofanyika Ukumbi wa Nkrumah wa chuo hicho mwishoni mwa wiki.
 Afisa wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Gasper Lyimo, akigawa fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko huo, kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, ambao walijiunga na Mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS
 Rais wa Serikali ya Wanafuzni wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, DARUSO,
Kitapenda Ahadi, (wakwanza kushoto), na makamu wake, Irene Deodatus Ishengoma, chini ya nusaidizi wa Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Rahma Ngassa, (wapili kushoto), na Mhamasishaji, Anthony Luvanda, (wapili kulia), wakijaza fomu za kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS
 Hadji Jamedary, Afisa wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akitoa mada kwa wanachuo wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, kuhusu umuhimu wa wanachuo hao kujiwekea akiba na hivyo kufaidika sasa na baadaye
 Sofia Abdallah, Mwanachuo wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, akipitia kijarida cha PSPF kinachoeleza kinaga ubaga shughuli na Mfuko na faida ambazo Mwanachama anapata
 Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba akitoa "darasa" kwa wasomi wa Mlimani

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Mwanaaikolojia Chris Mauki, akiwapa somo la "kujipanga" wanafunzi wa TUDACO
Afisa Masoko wa PSPF, Magire Werema akitoa mada kwa anafunzi wa TUDACO
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu Cha Tumaini kampasi ya Dar es Slaam, (TUDACO), akijaza fomu za kujiunga na PSPF, Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS
Mwanafunzi wa UDSM akipigwa picha ya kitambulisho baada ya kujiunga na Mpango wa PSS
Picha ya pamona baada ya semina ya Chuo Kikuu Cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam, (TUDACO)
Picha ya pamoja baada ya semina ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam pale Mlimani ukumbi wa Nkurumah
Albert Feruzi, akielezea huduma mbalimbali zitolewazo na PSPF wakati wa semina ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaa
Muhamasishaji, Anthony Luvanda, akitoa mada mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
Balozi wa PSPF, Mwanamitindo Flaviana Matata akizungumza na wanachuo wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

No comments: