Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Naibu Waziri Elimu Wazira wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe.
Mhandisi Stella Manyanya akijibu maswali kutoka kwa wabunge mbalimbali
katika kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Tano cha Bunge la
11 linaloendelea Mjini Dodoma Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi inatarajia
kujenga Vyuo vya Ufundi (VETA) kwa kila wilaya ili kutoa fursa kwa
wananchi wengi hususani vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ufundi
yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa.
Akijibu swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu ujenzi wa vyuo vya VETA kwa
kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja kati ya Wilaya kumi za
mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo hivyo wakati wa maswali na
majibu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe.
Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa
na Chuo Cha VETA sio kwa wilaya ya Chunya tu bali kwa Wilaya zote
nchini, tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni
pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika katika vyuo hivyo.
“ Natoa wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na
Halmashauri za Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa
ajili ya ujenzi wa vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute
eneo lipo tayari kwa kuanza utekelezaji wake”Alisema Mhe.Manyanya.
Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016
Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
imeshateua wataalamu elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la
jinsi ya kuifanya kazi ya kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo
ili kuanza ujenzi mara moja.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga
kutoa elimu bora ya ufundi yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya
ufundi stadi nchini ili kuwawezesha wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa
maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment