Social Icons

Friday, 5 February 2016

BALOZI SEIF AFUNGUA KINGAMANO LA VIJANA WA CCM WA VYUO VIKUU KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 39 YA KUZALIWA KWA CCM

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwenyekiti wa Vijana wa CCM wa Vyuo Vikuu Zanzibar kwa ajili ya kulifungua kongamano la CCM kutimia miaka 39 hapo Bwawani Hoteli Mjini Zanzibar.
Balozi Seif pamoja na Viongozi wengine wa ngazi ya Juu ya CCM na shirikisho la Vyuo Vikuu Tanzania wakifuatilia mambo yaliyokuwa yakiendelea kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 39 ya CCM ndani ya ukumbi wa Salama Bwawani.
Baadhi ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi walioshiriki Kongamano ya maadhimisho ya kutimia miaka 39 ya Chama cha Mapinduzi.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akilifungua Kongamano ya maadhimisho ya kutimia miaka 39 ya Chama cha Mapinduzi. Picha na – OMPR – ZNZ.
       
NA Othman Khamis Ame, OMPR 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba kazi kubwa iliyopo mbele kwa Vijana wa CCM wa Vyuo Vikuu ni kutafakari na kulipatia ufumbuzi tatizo la kupungua kwa ushindi wa Chama hicho ikilinganishwa na chaguzi nyengine zilizopita nyuma. 

No comments: