Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Meneja wa Habari , Elimu na
Mawasiliano Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Omega Ngole akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu
utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kuhusu upatikanaji wa mikopo
elimu ya juu uliofanyika Jijini Dar es salaam.
Meneja wa Habari , Elimu na
Mawasiliano Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Omega Ngole katikati akisisitiza jambo
mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wa kwanza kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Utoaji Mikopo Bw. Elias John
na wa kwanza kulia ni Afisa Mkuu wa Habari, Elimu na Mawasiliano Bi. Veneranda
Malima wakati wa kutoa utaratibu wa
kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kuhusu upatikanaji wa mikopo elimu ya juu
uliofanyika Jijini Dar es salaam.
Picha Na Ally Daud - Maelezo
Bodi ya Mikopo yatoa utaratibu wa
kuwasilisha malalamiko
Na jacquiline Mrisho –Maelezo
Dar es salaam
Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi wanaopata mikopo
katika taasisi za elimu ya juu nchini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano
Omega Ngole alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa
kushughulikia malalamiko ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.
“Utaratibu huu ulioboreshwa, ni msisitizo na
maelekezo ya Serikali ya mwezi Agosti 2011 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi ambayo ilielekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini
zinazopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kuanzisha Madawati ya Mikopo ili
kuongeza ufanisi katika utoaji mikopo”,Alisema Ngole.
Ameongeza
kuwa, dawati hilo linatakiwa kusimamiwa na mtumishi teule wa chuo husika mwenye
sifa na uhusiano mzuri na jamii na linapaswa kuwa chini ya Makamu Mkuu wa chuo
husika anayeshughulikia taaluma.
Meneja Ngole
amesisitiza kuwa kwa sasa vyuo vyote vina Maofisa Mikopo ambao wanawajibika
kutafuta suluhisho la suala linalowasilishwa na kulitolea majibu.
Akifafanua
hatua zinazotakiwa kufuatwa na Maofisa hao katika kutafuta suluhisho la
malalamiko ya wanafunzi amesema kuwa, baada ya malalamiko kufika kwa Ofisa
Mikopo yanatakiwa yapate suluhisho ndani ya siku mbili tangu kuwasilishwa
kwake,ikiwa hatakua na ufumbuzi atatakiwa kuwasiliana na uongozi wa juu wa chuo husika.
Endapo
uongozi wa juu wa chuo hautokuwa na ufumbuzi,
malalamiko hayo yatatakiwa kupelekwa kwenye Ofisi za Kanda ambazo zinapatikana
katika Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Arusha na Zanzibar au ofisi za makao ya makuu
ya Bodi zilizoko jijini Dar es Salaam.
Bodi ya
Mikopo ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi
mwezi Julai 2005 kwa majukumu ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji
waliodahiliwa katika Taasisi za Elimu ya Juu pamoja kukusanya marejesho ya
mikopo yote iliyotolewa tangu mwaka 1994.
No comments:
Post a Comment