Social Icons

Thursday, 14 January 2016

NACTE YAANDAA MKUTANO NA WAMILIKI WA VYUO BINAFSI NCHINI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma, na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa siku ya Ijumaa, tarehe 15/01/2016 saa mbili (2:00) asubuhi, kutakuwa na mkutano na wamiliki wote wa vyuo binafsi vyenye usajili wa Baraza, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kidini katika ofisi za NACTE  makao makuu, Mikocheni-Dar-es-Salaam.

Mkutano huo utaongelea mambo muhimu katika kuboresha sekta ya elimu ya ufundi nchini. Mkutano huo utafunguliwa na Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako (MB), Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Wamiliki/Meneja wote wa vyuo binafsi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi za kidini mnaombwa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa. Mialiko rasmi ya kimaandishi imeeletwa kwenu kupitia TAMONGSO, TAPIE, APHECOT, CSSC na BAKWATA.

Imetolewa na:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI


No comments: