Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa
Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe
29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima
ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo
tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais
Kikwete akimpongeza Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na
mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias walitumbuiza kwa wimbo wa
“Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote” kwa ufasaha na kusisimua
waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada
ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini
Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Kikwete na msafara wa wanachuo wakiondoka jukwaa kuu huku
wakishangiliwa na waliohudhuria ikiwa ni pamoja na Mama Salma Kikwete na
mwana wao Ali Kikwete na ujumbe wa Rais Kikwete kwenye msafara huo.
Sehemu ya umati wa wanachuo na wageni waalikwaa waliohudhuria sherehe
za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari
wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe
29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Sehemu
ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa
Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe
29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Mama
Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Rais
Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle
na mkewe Mama Salma Kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa
shahada.
Rais
Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe Mama
Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
Rais
Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali
Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete akipongezwa na raia wa Burundi waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.(PICHA NA IKULU).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia.
Sherehe za kumtunuku Rais shahada hiyo zimefanyika leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Newcastle.
Akisoma maelezo ya utangulizi katika
hafla hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans amesema
Rais Kikwete ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima
kutoka katika Chuo hicho.
Mkuu huyo wa Chuo amesema Rais Kikwete
ametunukiwa shahada hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kuleta
mabadiliko chanya duniani si kwa Tanzania tu bali kwa Dunia nzima kwani
mchango wake umetambulika na mashirika mbalimbali ya kimataifa
yakiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Benki ya Dunia kwa ujumla.
“Tangu kuingia madarakani Rais Kikwete amechangia katika kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu , uchumi na Afya” amesema Bw. Jean na kuongeza kuwa “utawala
wake umethibitishia sio Chuo cha Newcastle pekee bali pia kuonesha
kanuni ya Msingi kuwa Elimu ni muhimu katika kukuza uchumi, uvumbuzi na
katika maendeleo ya jamii” amesisitiza.
Tanzania imekua ikipokea misaada ya
elimu kutoka Australia katika nyanja mbalimbali zikiwemo za madini,
fedha, habari na tafiti mbalimbali ambazo zimeleta mabadiliko chanya
katika jamii na duniani kwa ujumla.
Kwa sasa Watanzania wanne wanachukua
masomo ya uzamifu katika masuala ya elimu na siasa.Tayari Watanzania 45
wamemaliza digrii na pia wapo watafiti kutoka Newcastle wanaofanya
tafiti zao nchini Tanzania katika masuala ya elimu, afya na uhandisi.
Rais Kikwete ameshukuru na kuelezea
jinsi alivyoguswa na tukio hilo ambapo ameushukuru uongozi wa Chuo hicho
kwa kutambua mchango wake ambao ameelezea kuwa ameufanya wakati wa
kipindi cha uongozi wake kwa moyo, upendo na nia njema kwa wananchi wote
wa Tanzania na Dunia kwa ujumla.
“Ilikua nia yangu na wajibu
wangu mkubwa kutumia ahadi nilizo waahidi wa Tanzania na hata zaidi ya
kile nilicho ahidi na kuelezea kuwa mafanikio haya yote yamechangiwa pia
kwa kiasi kikubwa na misingi imara iliyowekwa na viongozi
walionitangulia upande wa Tanzania bara na Tanzania Visiwani kwa ujumla”
Katika utawala wake Rais Kikwete
ametunukiwa shahada za heshima kutoka vyuo mbalimbali vya Marekani,
Canada, China, Uturuki na Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.
Rais Kikwete pia ametunukiwa tuzo za heshima mbalimbali katika masuala ya Kijamii (United Nations Social Good Award), Afya, Technolojia na Maendeleo (South-South Award for Global Health, Technology and Development) pamoja na Demokrasia (Icon of Democracy Award (Nertherlands)
Rais pia amepata kutunukiwa na kutambuliwa kwa Mchango wake ambapo alitunukiwa nishani kadhaa zikiwemo;
1.(Most Excellent Order of the Peral of Africa) ambayo ni nishani ya juu nchini Uganda.
2.The order of the Green Crescent of the Comoros (Comoros)
3.Order of Abdulazizi Al Saud (Saudi Arabia)
4.Order of excellence (Jamaica)
5. Order of Oman (Oman)
6. AAI African National Achievement Award
7. U.S. Doctors for Africa Award
8. Good Governance in Africa 2015
Sherehe hiyo imehudhuriwa na Mstahiki
Meya wa mji wa Newcastle, Mama Nuatali Nelmes, walimu na wakufunzi wa
Chuo cha Newcastle, wanafunzi wa Kitanzania na familia zao pamoja na
Watanzania kadhaa wanaoishi na kufanya kazi katika mji wa Newcastle.
Rais Kikwete amekamilisha ziara yake ya
Kiserikali ya siku nne nchini Australia na anatarajia kuelekea Dar-es
Salaam tarehe 30 Julai, 2015
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Newcastle-Australia
29 Julai, 2015
No comments:
Post a Comment