Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa mtandao wa FANPRAN,
Sithembile Ndema kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya
kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
JUMLA
ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika
kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha
miaka miaka mine iliyopita.
Hayo
yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo
Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa
akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa
uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.
Alisema
kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka
zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema
utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa
wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti
ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili
mabadiliko ya tabia nchi.
Profesa
Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha
Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya
maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili
mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es
salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni
ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto) huku wengine
wakishuhudia zoezi hilo, Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile
Ndema na wa pili kulia Mtafiti msaidizi kutoka ESRF, Ian Shanghvi.
Alitolea
mfano kuwa miradi ya kusambaza umeme vijijini ( REA) nchini ambayo
ilipata fedha nyingi katika miaka ya 2011 na 2012 ni miradi ya maendeleo
lakini hatima yake ni kuzuia ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya
nishati.
Akifafanua
fedha hizo zaidi alisema kwamba Tanzania mwaka 2010 jumuiya ya
kimataifa zilitoa dola za Marekani milioni 171.93, mwaka 2011 dola za
Marekani milioni 225.35, mwaka 2012 dola za Marekani milioni 229.74 na
mwaka 2013 Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 175.14.
Utafiti
huo ambao uligharamiwa na COMESA, EAC na SADC umewasilishwa katika
mkutano wa kitaifa wa uwezeshaji wa miradi ya kukabili tabia nchi kwa
mfumo wa ndani ambapo pia Mwakilishi wa mtandao wa FANRPAN, Sithembile
Ndema alikuwepo kuelezea maana ya mikutano ya kisera katika nchi
zinazounda mtandao huo.
Mtandao
huo ambao ulianzishwa mwaka 1994 baada ya mkutano wa mawaziri wa kilimo
wa nchi za SADC, EAC na COMESSA na makao makuu yake kuwa nchini
Zimbabwe ulianza kazi mwaka 1997 na sasa makao makuu yapo nchini Afrika
Kusini.
Mtandao
huo umelenga kuwezesha mataifa ya Afrika kuendesha kilimo na ufugaji
unaozingatia mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kutunza mazingira na
kuongeza tija.
Mikutano ya aina hiyo pia inafanyika Uganda, Ethiopia, Kenya na Zambia.
Profesa
Yanda alisema kwamba pamoja na fedha hizo kuonekana nyingi kiukweli ni
haba kutokana na hali halisi ilivyo sasa na hasa ikizingatiwa kwamba
kunatakiwa pia fedha za mabadiliko tabia nchi yenyewe badala ya kutumia
miradi ya maendeleo ambao matokeo ni kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Mshehereshaji
Hanif Tuwa kutoka ESRF, akitoa mwongozo wa yatakayojiri kwenye mkutano
wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia
nchi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za ESRF.
Alisema
takwimu walizopata kuhusu fedha zilizofika nchini kutoka katika jumuiya
ya kimataifa zililingana na taarifa zilizopo Hazina na kuonesha kwamba
fedha hizo zilienda kutumika katika makadirio yaliyokusudiwa.
“tofauti
iliyopo ni tafsiri ya miradi ya mabadiliko ya tabianchi. Miradi ya
maendeleo, inatamkwa kama miradi ya maendeleo lakini ukiangalia mwishoni
ni miradi hiyo kusaidia katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi”
alisema katika mahojiano baadae na na waandishi wa habari.
Alisema
kama Mkurugenzi wa Kituo cha mabadiliko ya tabia nchi anashauri
serikali kuhimiza wananchi wake kuendelea kusimamia mazingira vyema huku
wakulima na wafugaji wakisikiliza maofisa ugani kwa ajili ya kuwa na
kilimo na ufugaji bora usioharibu mazingira..
Alisema
tafiti mbalimbali zinaonesha kuwepo kwa athari kubwa ya mabadiliko ya
tabia nchi ambapo sasa hata sehemu za baridi za nyanda za juu zimeanza
kuwa na magonjwa ya Malaria huku wakulima wakiwa hawajui muda wa
kupanda kutokana na mabadiliko ya joto na pia unyeshaji wa mvua.
Alisema pia nyanda za juu sasa zinakabiliwa na wadudu waharibifu wa mazao vitu ambavyo awali havikuwepo.
Alisema
kwamba bado taifa linahitaji kufanya tafiti nyingi zaidi na kuzitumia
kuelimisha umma kuhusu nini kinatokea na nini kinastahili kufanywa
kukabili mabadiliko hayo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida akihutubia mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji
kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo umefanyika jana jijini Dar
es salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF na kujadili
taarifa ya utafiti uliofanywa kwa miaka minne kuhusiana na uwezeshaji.
Mkutano
huo wa kitaifa ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Taasisi huru ya Utafiti
wa Uchumi na Jamii (ESRF) Dk. Tausi Kida ambaye alisema lengo la mkutano
huo ni kuchambua utafiti uliofanywa na kuja na maazimio yatakayosaidia
kuboresha kilimo na kuhifadhi mazingira katika mapambano dhidi ya
mabadiliko ya tabia nchi.
Aliwaambia
washiriki kuiangalia kwa makini tafiti ya Profesa Pius Yanda na
kuhakikisha kwamba wanakuwa na uelewa wa maudhui na kuwezesha kutoa dira
ya utekelezaji katika siku za usoni.
Alisema
wakati taifa linajipanga kutekeleza mpango wake wa maendeleo wa
kuelekea katika uchumi wa viwanda suala la mabadiliko tabia nchi
haliwezi kuachwa na hivyo wajumbe wa mkutano walitakiwa kuangalia na
kuja na mapendekezo yao.
Mapendekezo
hayo ni pamoja na kuwa na kilimo na ufugaji wenye tija unazoingatia
ufanisi katika hifadhi ya mazingira na namna uwezeshaji wa ndani
unavyoweza kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema ni muhimu kilimo kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
ESRF
ni taasisi yinayojishughulisha na tafiti mbalimbali za jiuchumi na
kijamii zinazotoa mwelekeo wa utekelezaji wa sera na kanuni mbalimbali
za maendeleo na ustawi wa jamii.
Pmaoja
na kuratibu mkutano huo pia ilitoa nafasi ya ukumbi wake kutumika na
kutoa mwelekeo wa mkutano na umuhimu wake katika mpango wa pili wa
maendeleo wa taifa ambao unatakiwa uzingatie mabadiliko ya tabia nchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida akisoma hotuba na kuwakaribisha washiriki wa mkutano wa
kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi.
Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na kushoto ni
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es
salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda.
Mwakilishi
wa FANPRAN, Sithembile Ndema akielezea mradi wa COMESA wa uwezashaji wa
ndani wa fedha kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano
huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida (katikati) na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia
nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kulia)
wakifuatilia ka umakini 'presentation' ya Mwakilishi wa FANPRAN,
Sithembile Ndema (hayupo pichani).
Mkurugenzi
wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam
(UDSM), Prof. Pius Yanda, akitoa mada ya ufadhili wa kimataifa wa
uwezeshaji wa kifedha wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania katika mkutano
huo.
Pichani
juu na chini washiriki wakichangia mawazo yao kuhusu namna sera ya
uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi inavyopaswa kuwa katika
mkutano huo.
Pichani
juu na chini ni washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na
zisizo za serikali, watafiti, na wadau wa maendeleo waliohudhuria
mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya
tabia nchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa kitaifa
wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabianchi.
Picha ya pamoja ya washiriki.
No comments:
Post a Comment