Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Chuo cha Waislam
Morogoro kimeshiriki maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es
Salaam kilianzishwa mwaka 2005 na mpaka sasa kina miaka 10 kinatoa kozi mbalimbali kwa wanafunzi wanaojiunga katika chuo hicho. Afisa
mahusiano wa chuo cha Waislam Morogoro, Ngaja Mussa akimwonyesha
Mkufunzi mkuu wa chuo cha Waislam Morogoro, Faraji Tamim wakati wa maonyesho
ya wiki ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu nyerere
jinini Dar es Salaam.(Kwa hisani ya Michuzi Media)
Mkufunzi
wa chuo cha Waislam Morogoro wa Lugha ya Kichina katika chuo hicho, Sun
Xiaofei akizungumza na wateja mbalimbali waliotembelea katika maonyesho
ya vyuo vikuu vya hapa nchini na nje ya nchi.
Afisa
Udahili Yahya Mhando akitoa maelekezo kwa watu waliotembelea katika
banda la Chuo cha Waislam-Morogoro katika maonyesho ya wiki ya maonyesho
ya vyuo vikuu yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi
wa chuo cha Waislam Morogoro wa Lugha ya Kichina katika chuo cha
Waislamu Morogoro, Sun Xiaofei akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa shule
ya Sekondari Pugu walipotembelea katika maonesho ya wiki ya vyuo vikuu yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment