Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi
Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akitoa neno
kuwakaribisha wageni katika mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Vyuo vya Kodi Afrika
uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 50 kutoka katika taasisi za kodi barani
Afrika, Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na Taasisi za Kodi Afrika (ATAF), leo Jijini Dar es Salaam
Mkuu
wa Chuo cha Uongozi wa Kodi Tanzani (ITA) Prof. Isaiah Jairo akiongea na
wajumbe wa mkutano huo na kueleza namna utakavyosaidia katika kuzijengea uwezo
Taasisi za ukusanyaji kodi Afrika hivyo kuweza kuinua uchumi wa Mataifa mengi
ya Afrika.
Mkurugenzi
wa Ujengaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi
akiwaeleza wajumbe wa Mkutano huo namna Kamati hiyo inavyoshirikiana na Taasisi
za Kodi Afrika katika kuzijengea Taasisi hizo uwezo wa Kiutendaji na kusaidia
nchi wanachama kushiriki kuwa na sera ya pamoja ya masuala ya Kodi ili kuongeza
ufanisi katika ukusanyaji kodi.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba
Akiongea na wajumbe waliohudhuria Mkutano huo namna Tanzania
ilivyofurahishwa na kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa Kwanza wa wakuu wa vyuo vya uongozi wa Kodi Afrika na kuwataka
wajumbe kutumia fursa hiyo kujifunza masuala mbalimbali katika sekta hiyo ya
ukusanyaji kodi kwani ni moja ya mhimili muhimu wa maendeleo kwa Mataifa mengi
duniani.
Mkurugenzi Ujengeaji Uwezo kutoka Taasisi za
Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo
wa kwanza unaofanyika Nchini Tanzania
PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
No comments:
Post a Comment