Social Icons

Saturday, 6 December 2014

KINACHO ENDELEA SASA HIVI : MAHAFALI YA 49 YA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA(CBE) KAMPASI YA MBEYA


Mgeni rasmi katika Mahafali ya 49 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Musa Uledi, aliyemwakilisha Waziri wa Viwanda na biashara Dk. Abdalah Kigoda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kampasi ya Mbeya, akisaidiwa na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Emmanuel Mjema na Mwenyekiti wa Bodi Profesa Matthew Luhanga.

Katibu Mkuu akiingia Ofisini baada ya kukata utepe katika uzinduzi wa Chuo hicho.

Katibu Mkuu Musa Uledi sambamba na mwenyekiti wa Bodi Profesa Matthew Luhanga wakifunua kitambaa katika kibao kuashiria uzinduzi rasmi wa chuo cha Elimu ya Biashara katika kampasi ya Mbeya iliyopo Forest ya Zamani jijini Mbeya.


Katibu mkuu akiwasili Chuoni hapo tayari kwa uzinduzi wa Chuo Kampasi ya Mbeya.

Diwani wa kata ya Iganzo Uswege Furika akimkaribisha Katibu mkuu Musa Uledi alipotembelea eneo la Iganzo lenye ukubwa wa Ekari 55 lililotolewa na Wananchi kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya.

Diwani akiwaongoza wageni kuelekea sehemu ya eneo lililotolewa kwa ajili ya Chuo cha CBE

Chifu wa Iganzo Ndele Wilson akisalimiana na katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Musa Uledi.

Diwani wa Kata ya Iganzo, Uswege Furika akitoa taarifa kwa Katibu mkuu pamoja na viongozi alioongozana nao kutembelea eneo ambalo limetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Musa Uledi akizungumza na wananchi wa Kata ya Iganzo waliojitolea eneo lao kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara ambapo Katibu mkuu aliwapongeza.

Katibu wa Umoja wa Igomanzo Aman Mwazumba kutoka mitaa ya Iganzo na Igodima ambao ndiyo waliotoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Chuo akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Chifu akizungumza kwa niaba ya wananchi wa mitaa ya Iganzo na Igodima

Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wakiwa wamesimama kando kando ya eneo ambalo wamelitoa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo.

No comments: