Social Icons

Sunday 3 August 2014

MKUU WA MKOA WA IRINGA MH. DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) ATEMBELEA BANDA LA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA ( TIA) LEO, AFURAHISHWA NA HUDUMA.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Dr. Christine Ishengoma Akiwa anasaini katika kitabu cha wageni banda la TIA ndani ya maonesho ya Nane nane leo
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Dr. Christine Ishengoma akiwa anapata maelezo ya kujiunga na Chuo cha TIA pamoja na masomo yanayopatikana katika chuo hicho Bwana.Elimeleck P. Akyoo Mhadhiri msaidizi kutoka chuo hicho.
 Lilian Mpanju Rugatika Afisa Masoko na Masoko mwandamizi kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) akiwapa maelezo ya kina waliotembelea banda hilo maelezo juu ya kujiunga na chuo hicho fomu zinazopatikana na kuwasihi wajiunge kwa matunda Bora ya Elimu hapo baadae.a
 Watu mbalimbali wakiwa ndani ya Banda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA leo
 Bwana.Elimeleck P. Akyoo Mhadhiri msaidizi kutoka chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) akiendelea kutoa maelezo katika banda hilo.
 Bi. Lemeirut Mkuu wa Idara ya Uhasibu akiwa anatoa maelezo kwa watu mbalimbali waliotembelea Banda hilo akitoa maelezo ya Kujiunga na chuo hicho ikiwa ni pamoja na mwezi wa kuanza masomo hayo ambapo kwa mwaka huu ni Tarehe 1.09.2014
 Bi . Sanura Mohamed Mtunza Mahesabu Msaidizi wa Kumbukumbu  wa TIA akiwa anatoa maelezo kwa waliotembelea Banda lao.
 Bwana Mugisha Kyaruzi Kamala wa kwanza kutoka kulia ambaye ni Meneja wa Kampasi ya TIA mbeya akielezea juu ya Kampasi Hiyo.
 Banda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA 
 Baadhi ya vipeperushi.

*******
Meneja wa Tanzania Institute of Accountancy (TIA) Kampasi ya Mbeya anawatangazia wakazi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na wananchi wote kwa ujumla kutembelea banda la TIA katika Maonesho ya NANENANE yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale, Mkoani Mbeya.

Maelezo kuhusu Kozi za Cheti cha Awali (Basic Technician Certificates), Stashahada (Diploma), Shahada (Bachelor Degrees) na Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) kwenye fani za Uhasibu (Accountancy), Uhasibu wa Fedha za Umma (Public Sector Accounting & Finance), Ununuzi & Ugavi (Procurement & Logistics Management), Masoko na Uhusiano wa Umma (Marketing and Public Relations), Utawala wa Biashara (Business Administration)  na Raslimali Watu (Human Resource Management) yatatolewa. Pia fomu za kujiunga na chuo zinapatikana viwanjani kwa gharama ya sh. 20,000/= na malipo yanafanyika hapo viwanjani.

Kwa wale wanaokidhi vigezo, admission letters zinatolewa hapohapo. Mnashauriwa kuja na vivuli vya vyeti vyenu pamoja na picha (Passport size) moja.

Pia TIA inakusudia kuendesha kozi za Shahada (Bachelor Degrees) katika Kampasi ya Mbeya kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015 kwenye fani za Uhasibu na Ununuzi & Ugavi. (Mchakato wa kupata kibari toka  mamlaka husika unaendelea).

Fika kwenye banda letu lililopo katika viwanja vya TASO jirani na banda la Jiji.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia namba 0756273552 na 0753877652


“Kwa elimu yenye Ufanisi, jiunge na TIA”

Endelea kutembelea Mbeya yetu kujua zaidi juu ya TIA
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: